Wapotofu wanapindisha maana ya kulingana (اسْتَوَى) kwamba ni kutawala (استولى). Wameongeza herufi  (ل), ni kama jinsi mayahudi waliongeza  (ن) wakati Allaah alipowaamrisha kusema:

حِطَّةٌ

“Tuondolee uzito wa dhambi!”[1]

Lakini wakaongeza herufi (ن) na kusema:

حنطة

”Ngano.”

Ndipo Allaah (Ta´ala) akasema:

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ

”Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kutweza kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufuska.”[2]

´Ashaa´irah wameongeza herufi (ل) na mayahudi wakaongeza herufi (ن).

Isitoshe ni kwamba kutawala juu ya ´Arshi hakuna sifa maalum, kwani Allaah amekitawala kila kitu. Ni kwa nini mnafanya maalum ´Arshi? Jengine ni kwamba kukitawala kitu kunapelekea kwamba hapo kabla hakikuwa katika umiliki wake na kilikuwa katika umiliki wa mwengine. Ni kama inavosemwa kuwa ameshinda mfalme katika nchi fulani, wakimaanisha kuwa hapo kabla haikuwa katika umiliki wake. Ameitawala nchi hiyo baada ya kushinda. Shaykh-ul-Islaam ameibatilisha tafsiri hii kwa njia ishirini katika kitabu cha kujitegemea.

[1] 2:58

[2] 2:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 20/08/2024