Nao ndio ambao unatofautisha lile kundi jingine ambalo linayahifadhi Maandiko. Hamu yao ni kuyahifadhi na kuyadhibiti ambapo baadaye watu wakayaelekea na kuyachukua kutoka kwao. Baadaye wakazitolea hukumu, wakatoa humo hazina zake, wakazipanda katika ardhi inayofaa kupandwa na kuchipua na kila mmoja akayanywesha kwa kiwango chake:
قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ
”Kila kabila likajua mahali pake pa kunywea.”[1]
Hawa ndio wale ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwahusu:
“Allaah autie nuru uso wa mtu aliyesikia kutoka kwetu Hadiyth kisha akaifikisha kwa yule ambaye hakuisikia. Huenda mwenye kubeba uelewa asiwe mweleza, na huenda mwenye kubeba uelewa akamfikishia ambaye ni mweleza zaidi kuliko yeye.”[2]
Huyu hapa ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye ni mwanachuoni wa ummah na mfasiri wa Qur-aan, kiasi cha alichokisikia moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakikufikia hata Hadiyth ishirini, licha ya hivo amesikia mengi kutoka kwa Maswahabah na akawekewa baraka katika uelewa wake na uchukuaji wake hukumu kutoka humo mpaka akajaza ulimwengu wote kwa elimu na uelewa. Kwa mujibu wa Abu Muhammad bin Hazm fatwa zake zimekusanywa katika juzu saba kubwa[3]. Kwa msemo mwingine kwa mujibu wa yale yaliyomfikia mkusanyaji wake. La sivyo elimu ya Ibn ´Abbaas ni kama bahari. Aidha uelewa wake, kunyofoa kwake hukumu na ufahamu wake wa Qur-aan ni kwa kiwango ambacho alizidi watu wote. Amesikia kama walivyosikia wengine na akahifadhi Qur-aan kama walivyohifadhi wengine, lakini ardhi yake ilikuwa miongoni mwa ardhi nzuri kabisa na iliyo tayari kwa kupandwa. Matokeo yake Maandiko yakapandwa humo na zikatoa kila namna nzuri:
ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ
“Hiyo ni fadhilah ya Allaah humtunuku yule amtakaye – na Allaah ni Mwenye fadhilah kubwa.”[4]
[1] 2:60
[2] at-Tirmidhiy (2657), aliyesema kuwa ni nzuri na Swahiyh, Ibn Maajah (232) na Ahmad (2/148). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (89-91).
[3] al-Ihkaam fiy Usuwl-il-Ahkaam (5/92).
[4] 62:4
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 136-138
- Imechapishwa: 27/08/2025
Nao ndio ambao unatofautisha lile kundi jingine ambalo linayahifadhi Maandiko. Hamu yao ni kuyahifadhi na kuyadhibiti ambapo baadaye watu wakayaelekea na kuyachukua kutoka kwao. Baadaye wakazitolea hukumu, wakatoa humo hazina zake, wakazipanda katika ardhi inayofaa kupandwa na kuchipua na kila mmoja akayanywesha kwa kiwango chake:
قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ
”Kila kabila likajua mahali pake pa kunywea.”[1]
Hawa ndio wale ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwahusu:
“Allaah autie nuru uso wa mtu aliyesikia kutoka kwetu Hadiyth kisha akaifikisha kwa yule ambaye hakuisikia. Huenda mwenye kubeba uelewa asiwe mweleza, na huenda mwenye kubeba uelewa akamfikishia ambaye ni mweleza zaidi kuliko yeye.”[2]
Huyu hapa ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye ni mwanachuoni wa ummah na mfasiri wa Qur-aan, kiasi cha alichokisikia moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakikufikia hata Hadiyth ishirini, licha ya hivo amesikia mengi kutoka kwa Maswahabah na akawekewa baraka katika uelewa wake na uchukuaji wake hukumu kutoka humo mpaka akajaza ulimwengu wote kwa elimu na uelewa. Kwa mujibu wa Abu Muhammad bin Hazm fatwa zake zimekusanywa katika juzu saba kubwa[3]. Kwa msemo mwingine kwa mujibu wa yale yaliyomfikia mkusanyaji wake. La sivyo elimu ya Ibn ´Abbaas ni kama bahari. Aidha uelewa wake, kunyofoa kwake hukumu na ufahamu wake wa Qur-aan ni kwa kiwango ambacho alizidi watu wote. Amesikia kama walivyosikia wengine na akahifadhi Qur-aan kama walivyohifadhi wengine, lakini ardhi yake ilikuwa miongoni mwa ardhi nzuri kabisa na iliyo tayari kwa kupandwa. Matokeo yake Maandiko yakapandwa humo na zikatoa kila namna nzuri:
ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ
“Hiyo ni fadhilah ya Allaah humtunuku yule amtakaye – na Allaah ni Mwenye fadhilah kubwa.”[4]
[1] 2:60
[2] at-Tirmidhiy (2657), aliyesema kuwa ni nzuri na Swahiyh, Ibn Maajah (232) na Ahmad (2/148). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (89-91).
[3] al-Ihkaam fiy Usuwl-il-Ahkaam (5/92).
[4] 62:4
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 136-138
Imechapishwa: 27/08/2025
https://firqatunnajia.com/76-udongo-wa-ummah-usiyo-na-rutuba/