76. Ni ipi hukumu ya kutoa kiasi kikubwa cha fedha kuwapa makafiri?

Swali 76: Ni ipi hukumu ya kutoa kiasi kikubwa cha fedha kuwapa makafiri?

Jibu: Ikiwa ni kwa manufaa ya waislamu, basi hapana vibaya ili kuepuka shari yao. Hata zakaah inafaa kuwapa wale zinaolainishwa nyoyo zao katika makafiri kwa kutarajia kuzuia shari yao dhidi ya waislamu. Zakaah ambayo faradhi wanapewa makafiri kama hao. Kusemwe nini kuhusu pesa ambayo sio zakaah kwa ajili ya kuzuia madhara yao kwa waislamu? Baadhi ya wajinga hudhani kuwa kitendo hicho ni kuwapenda. Sio mapenzi. Huko ni kuwapa kitu cha kidunia kwa ajili ya kuwasalimisha waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 194
  • Imechapishwa: 17/07/2024