75. Kuchija wakati wa Hajj na Udhhiyah

Kuchinja Hadiy kwa mnasaba wa Hajj na Udhhiyah ni mambo mawili yanayopendeza muda wa kuwa mtu hajaweka nadhiri.

Kuchinja Udhhiyah ni bora kuliko kutoa swadaqah kwa thamani yake. Kilicho bora zaidi katika viwili hivyo ni ngamia, kisha ng´ombe, kisha mbuzi.

Inapendekezwa kuchagua wanyama wazuri na wanene.

Haifai isipokuwa kondoo wa mwenye miezi sita, na mwenye miaka miwili miongoni mwa wengine. Mbuzi mwenye miaka miwili ni yule aliyekamilisha mwaka mmoja, ngamia mwenye miaka miwili ni yule aliyekamilisha miaka mitano na ng´ombe ni yule mwenye miaka miwili.

Kondoo/mbuzi mmoja anatosheleza kwa mtu mmoja, na ngamia na ng´ombe mmoja anatosheleza kwa watu saba.

Haifai kumchinja mnyama mwenye jicho moja ambalo upofu wake unaonekana wazi, aliyekonda sana kiasi kwamba hana mafuta, mwenye kilema kinachoonekana wazi, mgonjwa ambaye ugonjwa wake unaonekana wazi na wala mnyama ambaye sehemu kubwa ya pembe au sikio lake imeondoka.

Anafaa mnyama asiye na pembe aliyezaliwa hivo, aliyekatwa mkia, amehasiwa na yule ambaye sikio lake limechanwa, kutobolewa au limekatwa chini ya nusu yake.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 50
  • Imechapishwa: 16/11/2026