74. Yanayopelekea kwa anayefanya Hajj aliyeacha nguzo au jambo la wajibu

Mwenye kuacha nguzo, basi ´ibaadah yake haitakamilika mpaka aitekeleze. Yule mwenye kuacha wajibu, basi atairekebisha kwa kuchinja mnyama wa fidia. Ambaye ataacha jambo linalopendeza, basi hakuna chochote kinachomlazimu.

Ambaye hakusimama ´Arafah mpaka alfajiri ya siku ya kuchinja ilipochomoza, basi Hajj yake imempita. Hivyo basi hutoka katika Ihraam kwa kufanya Twawaaf na Sa´y, na huchinja Hadiy ikiwa yuko naye. Baada ya hapo anawajibika kuja kufanya Hajj hiyo baadaye.

Ikiwa watu watakosea katika kuhesabu tarehe ambapo wakasimama katika siku nyingine isiyo siku ya ´Arafah, basi itawatosheleza. Lakini ikiwa ni kundi la watu ndio watafanya kosa hilohilo, basi Hajj yao itakuwa imewapita.

Inapendekezwa kwa mwenye kufanya Hajj kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makaburi ya Maswahabah wake wawili – Allaah awe radhi nao!

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 16/11/2026