Ni Sunnah kumchinja ngamia akiwa amesimama, huku mguu wake wa mbele wa kushoto ukiwa umefungwa, na kuchinja ng´ombe na mbuzi wakiwa wamelazwa ubavuni. Wakati wa kufanya hivo aseme:
بسم الله ، و الله أكبر، اللهم إن هذا منك و لك
“Naanza kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa. Ee Allaah! Hii imetoka Kwako na ni kwa ajili Yako.”[1]
Haipendekezwi kuchinjwa na mwengine isipokuwa na aliye muislamu. Mnyama akichinjwa na mwenye nao ndio bora zaidi.
Wakati wa kuchinja ni siku ya ´Iyd baada ya swalah ya ´Iyd mpaka mwisho wa siku mbili za Tashriyq.
Udhhiyah inakuwa maalum kwa kusema kwake “Hii ni Udhhiyah.” Mnyama wa Hadiy inakuwa maalum kwa kusema kwake “Hii ni Hadiy”, pamoja na kumuweka alama kunahitaji nia.
Asimpe mchinjaji chochote katika Udhhiyah kama malipo ya kazi yake.
Sunnah ni kula theluthi moja ya Udhhiyah yake, kutoa zawadi theluthi yake na kutoa swadaqah theluthi yake. Ikiwa atakula zaidi, inafaa. Anaruhusiwa kunufaika na ngozi yake. Hata hivyo asiiuze wala asiuze chochote miongoni mwake.
Inapokuja katika mnyama wa Hadiy, ikiwa ni wa kujitolea, basi inapendekezwa kwake kula sehemu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamuru wachukue kipande cha kila ngamia, kikapikwa, kisha akala nyama yake na akanywa mchuzi wake. Wala hali kutoka katika mnyama wa Hadiy wa wajibu isipokuwa Hadiy ya mwenye kufanya Hajj ya Tamattu´ na Hajj ya Qiraan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote mwenye kutaka kuchinja Udhhiyah, kisha kumi la kwanza likaanza, basi asikate chochote katika nywele wala katika ngozi yake mpaka achinje.”[2]
[1] Abu Daawuud (2795). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (1152).
[2] Muslim (1977).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 50
- Imechapishwa: 16/11/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 50
Imechapishwa: 16/11/2026
https://firqatunnajia.com/76-vigezo-na-adabu-za-uchinjaji/