Mfano wa pili wa majimaji ni katika maneno Yake (Ta´ala):
أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ
”Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni ndani yake kuna viza na radi na umeme; wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakichelea kifo; na Allaah ni Mwenye kuwazunguka makafiri.”[1]
Dhoruba kali ni mvua inayomiminika kutoka mbinguni. Huo ndio mfano wa Qur-aan ambayo ndani yake kuna uhai wa nyoyo, kama mvua inavyotoa uhai kwa ardhi, mimea na wanyama. Waumini wameufahamu huo mfano na wakajua yanayopatikana kwayo ya uhai ambao hauingii akilini. Hawakuzuiwa nayo na yale yaliyomo ndani yake ya radi na umeme, ambayo kunakusudiwa maonyo, vitisho, adhabu na mateso ambayo Allaah ameonya kwa anayekiuka amri Yake na akakhabarsha kuwa atawateremshia wale waliomkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au yale yaliyomo ndani yake ya amri ngumu, kama vile jihaad dhidi ya maadui, subira juu ya amri au amri ngumu kwa nafsi ambazo ni kinyume na matakwa yao. Kwa hiyo hayo ni kama giza, radi na umeme. Lakini yule anayejua maeneo ya mvua na yanayopatikana kwayo katika uhai, haogopi yaliyomo humo katika giza, radi na umeme. Bali huona faraja kwa hivyo na hufurahia kwa sababu ya kutarajia kwa ajili yake uhai na ustawi.
[1] 02:19
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 128
- Imechapishwa: 25/08/2025
Mfano wa pili wa majimaji ni katika maneno Yake (Ta´ala):
أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ
”Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni ndani yake kuna viza na radi na umeme; wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakichelea kifo; na Allaah ni Mwenye kuwazunguka makafiri.”[1]
Dhoruba kali ni mvua inayomiminika kutoka mbinguni. Huo ndio mfano wa Qur-aan ambayo ndani yake kuna uhai wa nyoyo, kama mvua inavyotoa uhai kwa ardhi, mimea na wanyama. Waumini wameufahamu huo mfano na wakajua yanayopatikana kwayo ya uhai ambao hauingii akilini. Hawakuzuiwa nayo na yale yaliyomo ndani yake ya radi na umeme, ambayo kunakusudiwa maonyo, vitisho, adhabu na mateso ambayo Allaah ameonya kwa anayekiuka amri Yake na akakhabarsha kuwa atawateremshia wale waliomkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au yale yaliyomo ndani yake ya amri ngumu, kama vile jihaad dhidi ya maadui, subira juu ya amri au amri ngumu kwa nafsi ambazo ni kinyume na matakwa yao. Kwa hiyo hayo ni kama giza, radi na umeme. Lakini yule anayejua maeneo ya mvua na yanayopatikana kwayo katika uhai, haogopi yaliyomo humo katika giza, radi na umeme. Bali huona faraja kwa hivyo na hufurahia kwa sababu ya kutarajia kwa ajili yake uhai na ustawi.
[1] 02:19
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 128
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/71-usiogope-giza-radi-na-umeme/