70 – ath-Thawriy na wengine pia wameipokea kupitia kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa Abuz-Za´raa´, kutoka kwa ´Abdullaah kwa tamko lisemalo:

”Allaah atajidhihirisha kwa viumbe kisha Awajilie kwa sura Yake.”

Haya yamesihi kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd[1].

Ishaaq bin at-Twabbaa´ amepokea kwamba kulisemwa kuambiwa ´Abdul-´Aziyz bin al-Maajashuun:

”Allaah ni mtukufu na ni mkubwa zaidi kwa Yeye kuonekana namna hii.” Ndipo akasema: ”Ee mpumbavu! Si kwamba ukubwa[2] wa Allaah ndio unabadilika, isipokuwa ni macho yako, mpaka ukaweza kumuona Anavyotaka.”

[1] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia wao. Kupitia al-Bukhaariy na Muslim wameipokea jopo kubwa akiwemo Ibn Khuzaymah katika “Kitaab-ut-Tawhiyd”, uk. 113-115, na al-Bayhaqiy, katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 291-296.

[2] Imekuja namna hii katika zile zote za asili. Katika “al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn” imekuja ”sifa Yake”. Pengine hivi ndio sahihi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 111
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy