Swali 70: Ikiwa mwanafunzi yuko na Bid´ah na analingania kwayo na wakati huohuo akawa ni mjuzi wa Fiqh na Hadiyth. Je, elimu zake zote zinadondoka kwa sababu ya Bid´ah yake? Haifai kabisa kumtumia kama hoja?

Jibu: Ni kweli. Haaminiki. Ikiwa ni mzushi na anaonyesha waziwazi Bid´ah zake haaminiki. Haitakiwi kusoma kwa mtu kama huyo. Kwa sababu kukisomwa kwake wanafunzi wake wataathirika na mwalimu wao na elimu yake. Kwa hivyo ni lazima kujitenga mbali na Ahl-ul-Bid´ah. Salaf walikuwa wakikataza kukaa na Ahl-ul-Bid´ah, kuwatembelea na kwenda kwao kwa kuchelea kutoenea shari yao kwa yule ambaye anakaa na kuchanganyika naye[1].

[1] Matangamano na kuchanganyika ni mambo yanaathiri. Abu Dharr al-Harawiy aliathirika kwa Abu Bakr bin at-Twayyib. Baada ya kwenda kwake mara kwa mara akachukua ´Aqiydah yake ya Ashaa´irah.

Mfano mwingine ni ´Imraan bin Hittwaan aliyesimulia kutoka kwa kikosi kikubwa cha Maswahabah na hapo kabla alikuwa katika Ahl-us-Sunnah. Lakini matangamano yake yakamfanya kujiunga na Khawaarij. Ya´quub bin Shaybah amesema:

”Tulifikiwa na khabari kuwa sababu ya hilo ni kwamba binamu yake wa kike alikuwa anaona maoni ya Khawaarij. Akamuoa ili amrudishe kutokana na hilo. Badala yake mwanamke huyo akamgeuza kwenda katika ´Aqiydah yake.” (Tahdhiyb-ut-Tahdhiyb (8/113))

Hakuna ushahidi mkubwa unaothibitisha kuwa matangamano yanaathiri kama ya yule ambaye hatamki kwa matamanio yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa  sallam):

”Mtu yuko katika dini ya rafiki yake. Hivyo basi, aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya rafiki.” (as-Swahiyhah (927))

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 177
  • Imechapishwa: 03/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy