Jubayr bin Nufayl amesimulia kutoka kwa ´Awf bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye ameeleza:
”Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitazama juu mbinguni akasema: ”Umefika wakati wa kuenuliwa elimu.” Bwana mmoja katika Wanusuraji, kwa jina la Ziyaad bin Labiyb, akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Itainuliwa elimu ilihali imekwishathibiti na kueleweka na nyoyo?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: ”Nilikuwa nafikiri wewe ndiye mjuzi zaidi katika watu wa Madiynah.” Kisha akataja upotofu wa mayahudi na manaswara licha ya Kitabu cha Allaah walichonacho. Baadaye nikakutana na Shaddaad bin Aws ambapo nikamweleza Hadiyth ya ´Awf bin Maalik. Akasema: ”´Awf amesema kweli. Je, nisikujuze kitu cha kwanza katika hayo kitachonyanyuliwa?” Nikasema: ”Ndio.” Akasema: ”Unyenyekevu. Hutomuona yeyote ambaye ananyenyekea.”[1]
Ameipokea an-Nasaa´iy.
Jubayr amesema:
“Nilikutana na ‘Ubaadah bin as-Swaamit na nikasema: “Je, husikii yale yanayosemwa na ndugu yako Abud-Dardaa’?” Nikamweleza yake yanayosemwa na Abud-Dardaa’, ambapo akasema: “Abud-Dardaa’ amesema ukweli. Ukitaka naweza kukwambia ile elimu ya kwanza inayonyanyuliwa kutoka kwa watu; unyenyekevu. Unakaribia kuingia msikiti wa mkusanyiko na usimkute ndani yake yeyote anayenyenyekea.”[2]
Ameipokea at-Tirmidhiy. Inasemekana kuwa upokezi wa an-Nasaa´iy ndio wenye nguvu zaidi.
Sa’iyd bin Bashir al-Hasan (Rahimahu Allaah) kutoka kwa Shaddaad bin Aws, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Kitu cha kwanza kitachonyanyuliwa kutoka kwa watu ni unyenyekevu.”
Abu Bakr bin Abiy Maryam ameipokea kutoka kwa Hamzah bin Habiyb bila ya Swahabah kwenye cheni ya wapokezi. Amepokea pia mfano wake kutoka kwa Hudhayfah.
[1] an-Nasaa’iy (8/211), Ahmad (6/26), Ibn Hibbaan (115) na al-Haakim (1/99), ambaye ameisahihisha. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal” (89).
[2] at-Tirmidhiy (2653), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni. Swahiyh kwa mujibu al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2653).
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 43-46
- Imechapishwa: 24/11/2025

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 43-46
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/7-wakati-unyenyekevu-unapoanza-kupungua/