Basi hebu mwenye akili atafakari Aayah hii tukufu na jinsi inavyolingana na maana hizi tukufu. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ametaja nuru Yake katika mbingu na ardhi na nuru Yake katika nyoyo za waja Wake waumini. Ni nuru inayofahamika na inayoonekana kwa macho ya moyo na nyoyo. Ni nuru ya kimwili inayoonekana kwa macho ambayo imeangaza pembe zote za ulimwengu wa juu na wa chini. Basi hizi ni nuru mbili tukufu ambapo moja ni kubwa zaidi kuliko nyingine.
Ikiwa nuru moja itakosekana katika mahali au sehemu, basi hakuna mwanadamu au kiumbe kingine atakayeishi mahali hapo. Viumbe huishi mahali ambapo kuna nuru. Hakuna yeyote anayeishi maeneo pa giza na mahali ambapo hakuna nuru. Vivyo hivyo pia ummah ambao hauna nuru ya wahy na imani ni ummah uliokufa. Moyo ambao ndani yake hakuna nuru hii ni moyo uliokufa na wala hauna maisha kabisa, kama vile kiumbe kisivyoweza kuishi mahali pasipo na nuru. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anahusianisha kati ya uhai na nuru, kama pale aliposema (´Azza wa Jall):
أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَاَ
“Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamuhuisha na tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yuko katika viza si mwenye kutoka humo?”[1]
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
”Na hivyo ndivyo tulivyokuletea Roho katika amri Yetu. Hukuwa unaelewa nini Kitabu na wala imani, lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.”[2]
Kuna mitazamo ya maoni tofauti kuhusu kiwakilishi katika maneno Yake (´Azza wa Jall):
وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا
”Lakini tumeifanya kuwa ni nuru… ”
Kuna maoni yanayosema kwamba kunakusudiwa Kitabu. Mengine yanasema kuwa kunakusudiwa imani. Hata hivyo sahihi ni kunakusudiwa roho. Kwa maana nyingine ni kuwa Tumeifanya roho hiyo ambayo tumeiteremsha kwako kuwa ni nuru. Ameiita kuwa ni roho kutokana na ule uhai unaopatikana kwayo, na akaifanya nuru kwa sababu hupatikana nayo mwangaza na mwangavu. Vitu viwili hivi vinaenda sambamba. Mahali panapopatikana uhai huu kupitia roho, basi hapohapo hupatikana mwangaza na mwangavu. Mahali panapopatikana mwangaza na mwangavu, basi hupatikana pia uhai. Basi yule asiyeikubali roho hii ni mfu wa giza kama mtu ambaye mwili wake unapoteza roho ya uhai.
[1] 6:122
[2] 42:52-53
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 123-125
- Imechapishwa: 25/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 123-125
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/68-uhai-na-nuru/