67. ´Arshi imetikisika wakati alipokufa

64 – Anas ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati ambapo jeneza la Sa´d lilikuwa tayari kwa ajili ya kuswaliwa: ”´Arshi ya Mwingi wa rehema imetikisika kwa ajili yake.”[1]

Hii ni Swahiyh.

65 – Abu Sa´iyd amesimulia ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”´Arshi ilitikisika kwa ajili ya kifo cha Sa´d bin Mu´aadh.”[2]

Hadiyth hii ni Swahiyh.

66 – Usayd bin Hudhwayr amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”´Arshi ilitikisika juu ya kifo cha Sa´d.”

Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

67 – Rumaythah amesema:

”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema – na ningelitaka kubusu muhuri wake kwa jinsi nilivyokuwa karibu basi ningelifanya: ”Imetikisika ´Arshi ya Mwingi wa huruma.”

Akimkusudia Sa´d bin Mu´aadh. Cheni hii imesalimika[3]. Ibn Mandah ameisahihisha. Hadiyth hiyohiyo imesimuliwa na Sa´d bin Abiy Waqqaas, Ibn ´Umar, Hudhayfah, Abu Hurayrah, Asmaa’ bint Yaziyd na Mu´ayqiyb. Kwa hiyo yamepokelewa kwa mapokezi tele. Nashuhudia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyasema.

[1] Muslim na wengineo. Tazama “Dhwilaal-ul-Jannah” (561).

[2] Ahmad na Ibn Sa´d. Tazama “Dhwilaal-ul-Jannah” (564-567).

[3] Hili linahitaji kuangaliwa vyema, kama nilivyobainisha katika “Dhwilaal-ul-Jannah” (567). Katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” (1/137-138 – muswada) kuna mlango maalum juu ya Hadiyth hii. Humo amekusanya cheni za wapokezi za Hadiyth hiyo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy