al-Qummiy amesema:
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]
“Aayah hii inahusiana na familia ya Muhammad na wafuasi wao. Wanalingania katika kheri na wanaamrisha mema na kukataza maovu.”[2]
Aayah hii inaamrisha Ummah mzima kuamrisha mema (ambayo ni Tawhiyd, ´Aqiydah sahihi na matendo mema yaliyoamrishwa na Allaah) na kukataza maovu (ambayo ni shirki, upotevu, Bid´ah na kila dhambi kubwa na ndogo yenye kukhalifu Shari´ah ya Allaah).
Hii ni sifa ya kipekee ya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kukiwepo baadhi ambao watasimama na wajibu huu basi wengine hawana uwajibu wa kufanya hivo. Wakipuuzia hilo basi majukumu wanabeba wote. Kusema kwamba Aayah hii inahusiana na familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wafuasi wao ni kumsemea uongo Allaah na ni kuyapotosha maneno ya Allaah. Hii ndio kazi ya mayahudi. Uhakika wa mambo ni kwamba Raafidhwah hawafuati kabisa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanamfuata myahudi Ibn Sabaa´ na makamanda wake katika Raafidhwah na mazanadiki ambao wana mfumo mmoja kama Ibn Sabaa´. Wanalingania katika maovu, shirki, ukafiri na upotevu. Wao ni maadui wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na kizazi chake.
[1] 03:104
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/109).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 104
- Imechapishwa: 03/04/2017
al-Qummiy amesema:
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]
“Aayah hii inahusiana na familia ya Muhammad na wafuasi wao. Wanalingania katika kheri na wanaamrisha mema na kukataza maovu.”[2]
Aayah hii inaamrisha Ummah mzima kuamrisha mema (ambayo ni Tawhiyd, ´Aqiydah sahihi na matendo mema yaliyoamrishwa na Allaah) na kukataza maovu (ambayo ni shirki, upotevu, Bid´ah na kila dhambi kubwa na ndogo yenye kukhalifu Shari´ah ya Allaah).
Hii ni sifa ya kipekee ya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kukiwepo baadhi ambao watasimama na wajibu huu basi wengine hawana uwajibu wa kufanya hivo. Wakipuuzia hilo basi majukumu wanabeba wote. Kusema kwamba Aayah hii inahusiana na familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wafuasi wao ni kumsemea uongo Allaah na ni kuyapotosha maneno ya Allaah. Hii ndio kazi ya mayahudi. Uhakika wa mambo ni kwamba Raafidhwah hawafuati kabisa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanamfuata myahudi Ibn Sabaa´ na makamanda wake katika Raafidhwah na mazanadiki ambao wana mfumo mmoja kama Ibn Sabaa´. Wanalingania katika maovu, shirki, ukafiri na upotevu. Wao ni maadui wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na kizazi chake.
[1] 03:104
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/109).
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 104
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/67-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-sita-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)