Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Mayahudi na manaswara ndio watu wa Kitabu na wamegawanyika sampuli mbili:

1 – Wanaomuamini Allaah na Mtume Wake na wakamtii Allaah. Miongoni mwao wako ambao wamekufa kabla ya kutumilizwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walikuwa wema na wanaowaamini Mitume. Wengine wakakutana na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakamuamini. Hawa wamepata ujira mara mbili: ujira wa kuwafuata Mitume walitoangulia na ujira mwingine wa kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

 “Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na muaminini Mtume Wake! Hapo atakupeni sehemu mbili kati ya rehema Zake na atakujaalieni nuru mnatembea nayo na akusameheeni; Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Hii inawahusu manaswara na mayahudi.

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ

”Hawako sawasawa. Miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab wako watu wenye kusimama, wanasoma Aayah za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu.”[2]

وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ

”Na miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab wamo ambao kwa hakika wanamwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah, na hawabadilishi Aayah za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Mola wao. Hakika Allaah Ni Mwepesi Mno wa Kuhesabu.”[3]

Hawa ni waumini katika watu wa Kitabu.

2 – Wale waliowakufuru Mitume na wakabadilisha, wakapotosha na kugeuza Tawraat na Injiyl. Hii ndio hali ya mayahudi na manaswara wengi.

[1] 57:28

[2] 3:113

[3] 3:199

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 13/08/2024