Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
2 – Atawaombea watu wa Peponi waingie Peponi.
Nyombezi hizi mbili ni maalum kwake.
3 – Atawaombea wale waliostahiki kuingia Motoni. Na uombezi huu ni kwake na kwa Mitume wengine, wakweli mno na wengineo. Atawaombea wale waliostahiki kuingia Motoni wasiingizwe na awaombee wale walioingia watolewe humo. Allaah (Ta´ala) atawatoa ndani ya Moto watu, si kwa sababu ya uombezi, bali ni kwa sababu ya fadhilah na huruma Yake.
Kutabaki Peponi nafasi baada ya watu walioingia na Allaah ataumba watu maalum kwa ajili yake kisha awaingize Peponi.
MAELEZO
Atawaombea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakazi wa Peponi ili waingizwe Peponi. Atawaombea watu walioingia Motoni kwa sababu ya madhambi na maasi yao baada ya Allaah kuwaadhibu awaondoshe Motoni. Atawaombea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mara nne, kila mara atapoombea kutatolewa idadi kadhaa ya waliomuasi Allaah, kama ilivyosihi[1].
Mitume, waumini na watoto wa kiislamu waliokufa kabla ya kubaleghe wataombea. Mambo ni kama alivosema mtunzi wa kitabu, ufafanuzi juu ya yatayopitika siku ya Qiyaamah, ni jambo zito. Watabaki Motoni baadhi ya wapwekeshaji ambao hawakupata uombezi. Hawa ni wale watenda madhambi waliokuwa wakimuabudu Allaah peke yake ambao wameingia Motoni kwa sababu ya madhambi yao. Hata hivyo Allaah (Jalla wa ´Alaa) atawatoa Motoni kwa fadhilah na huruma Yake pasi na uombezi wa yeyote. Hawa ndio wataokuwa wamebaki Motoni na watakuwa wameungua na Moto. Baada ya hapo watawekwa kwenye mto wa Uhai na wachipuke kama inavyochipuka mbegu kwenye takataka za mafuriko. Litapotimia umbile lao Allaah atawaingiza Peponi kwa fadhilah na rehema Zake (Subhnaanahu wa Ta´ala).
[1] al-Bukhaariy (6565) na Muslim (192).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 97-98
- Imechapishwa: 02/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)