5 – Asmaa´ bint Abiy Bakr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Tulikuwa tukifunika nyuso zetu kutokana na wanamme. Kabla ya hapo tulikuwa tukichana kwa ajili ya Ihraam.”[1]

[1] Ameipokea al-Haakim (1/454) na akasema kuwa Hadiyth ni Swahiyh kwa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Hata hivyo Hadiyth ni kwa mujibu wa sharti za Muslim peke yake, kwa sababu hakumpokea Zakariyyaa bin ´Adiy katika cheni ya wapokezi katika “al-Jaamiy´ as-Swahiyh” yake isipokuwa ni katika vitabu vingine, kama ilivyotajwa katika ”at-Tahdhiyb”. Maalik amepokea mfano wake kutoka kwa Faatwimah bint al-Mundhir.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 108
  • Imechapishwa: 05/10/2023