60 – ´Ubaadah bin as-Swaamit amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Pepo ina ngazi mia. Umbali kati ya ngazi mbili ni kama mfano wa umbali wa mbingu na ardhi. Firdaws ndio yenye ngazi ya juu zaidi. Juu yake kuna ´Arshi. Mkimuomba Allaah, basi mwombeni Firdaws.”

Wameipokea wasimulizi madhubuti. Kumeshatangulia mfano wake kutoka kwa Abu Hurayrah. Nayo ndio Swahiyh zaidi[1].

[1] Bali cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh, kama alivosema al-Haakim na mtunzi katika ufupisho wake. Ingawa ameashiria kuwa Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia ndio Swahiyh zaidi, naonelea, kama Haafidhw Ibn Hajar, kwamba Hadiyth zote mbili ni Swahiyh, kama nilivyobainisha katika ”as-Swahiyhah” (921). Hadiyth imepokelewa pia na Ahmad na at-Tirmidhiy.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 107
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy