Download

169-

اللّهُمَّ اَسْقِـنا غَيْـثاً مُغيـثاً، مَريئاً، مُريـعاً، نافِعـاً غَيْـرَ ضَّارٌ، عاجِـلاً غَـيْرَ آجِلٍ

”Ee Allaah! Tunyesheleze mvua yenye kusaidia, nzuri, yenye manufaa isiyo dhuru, ya haraka isiyochelewa.”[1]

 170-

اللّهُمَّ أغِثْنـَا، اللّهُمَّ أغِثْنـَا، اللّهُمَّ أغِثْنـَا

“Ee Allaah! Tunakuomba utuokoe kwa kututeremshia mvua. Ee Allaah! Tunakuomba utuokoe kwa kututeremshia mvua. Ee Allaah! Tunakuomba utuokoe kwa kututeremshia mvua.”[2]

171-

اللّهُمَّ اسْقِ عِبادَكَ وَبَهـائِمَك، وَانْشُـرْ رَحْمَـتَكَ وَأَحْيِي بَلَـدَكَ المَيِّـت

“Ee Allaah! Wanyesheleze waja Wako na wanyama Wako na zieneze rehma Zako na ufufue nchi Yako iliyokufa.”[3]

[1] Abu Daawuud (01/303). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (01/216).

[2] al-Bukhaariy (01/224) na Muslim (02/612).

[3] Abu Dawuuud (01/305). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuwd” (01/218).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/05/2020