Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Mtu wa kwanza ambaye ataomba idhini ya kuingia Peponi ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1] na watu wa kwanza ambao wataingia Peponi ni ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[2].
MAELEZO
Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameamrisha asifunguliwe yeyote mlango kabla yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye mtu wa kwanza atayefunguliwa mlango wake na kubisha hodi mlango wake. Mlinzi wa Pepo atamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Niliamrishwa nisimfungulie yeyote mlango kabla yako.”[3]
Ee Allaah msifu na msalimishe! Ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio utakuwa wa kwanza kuingia Peponi. Baada ya Mitume ummah bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ummah wa kwanza miongoni mwa nyumati utaoingia Peponi na ulio bora baada ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) ni ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (197).
[2] Muslim (855).
[3] Muslim (197).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 94-95
- Imechapishwa: 02/11/2024
Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Mtu wa kwanza ambaye ataomba idhini ya kuingia Peponi ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1] na watu wa kwanza ambao wataingia Peponi ni ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[2].
MAELEZO
Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameamrisha asifunguliwe yeyote mlango kabla yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye mtu wa kwanza atayefunguliwa mlango wake na kubisha hodi mlango wake. Mlinzi wa Pepo atamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Niliamrishwa nisimfungulie yeyote mlango kabla yako.”[3]
Ee Allaah msifu na msalimishe! Ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio utakuwa wa kwanza kuingia Peponi. Baada ya Mitume ummah bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ummah wa kwanza miongoni mwa nyumati utaoingia Peponi na ulio bora baada ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) ni ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (197).
[2] Muslim (855).
[3] Muslim (197).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 94-95
Imechapishwa: 02/11/2024
https://firqatunnajia.com/62-mtu-wa-kwanza-kuingia-peponi/