Kusoma kwa zamu kwa Qur-aan ni pale kundi linapokusanyika, mmoja wao anasoma Aayah kumi au juzu au kiasi kingine, kisha anyamaze na mwingine asome kuanzia alipoishia wa kwanza na kadhalika. Hili linajuzu na ni jema. Maalik (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu mfumo huu ambapo akasema:

”Hakuna vibaya.”

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 65
  • Imechapishwa: 23/11/2026