ad-Daarimiy amepokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye amesema:
“Anayesikiliza Aayah kutoka katika Kitabu cha Allaah, basi huwa ni nuru kwake.”[1]
Ibn Abiy Daawuud amepokea:
”Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akijifunza Qur-aan pamoja na kundi la watu ambapo wakisoma wote kwa pamoja.”
Ibn Abiy Daawuud amepokea jinsi vitendo vya kujifunza Qur-aan kwa pamoja kutoka kwa makundi ya wanazuoni bora wa Salaf, waliokuja baada yao na hata miongoni mwa mahakimu wa mwanzo vilivyokuwa vizuri. Hassaan bin ´Atwiyyah na al-Awzaa´iy wamesema:
”Mtu wa kwanza kuanzisha utaratibu wa kusoma Qur-aan katika msikiti wa Dameski alikuwa Hishaam bin Ismaa’iyl wakati alipofika kwa ´Abdul-Malik.”
Ama yale yaliyopokelewa na Ibn Abiy Daawuud kwamba adh-Dhwahhaak bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Arzab alipinga usomaji wa mfumo huu na akasema:
”Sijaona na wala sijasikia ilihali nimewaona Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Kwa maana ya kwamba hajamuona yeyote akifanya namna hiyo.
Ibn Wahb amesema:
”Nilimwambia Maalik: ”Unaonaje watu wanakusanyika wakasoma pamoja Suurah moja mpaka waimalize?” Akapinga jambo hilo na kulichukia na akasema: ”Si hivyo watu walivyokuwa wakifanya. Bali mtu alikuwa akimsomea mwengine.”
Upingaji wao huu unapingana na yale waliyokuwa nayo Salaf na waliokuja baada yao na yale yanayopelekea dalili na kwa ajili hiyo kunatupiliwa mbali na tegemeo ni yale yaliyotangulia ya kupendekezwa kwake. Lakini kusoma katika hali ya kukusanyika kuna masharti tuliyotanguliza ambayo yanapaswa kuzingatiwa – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
Ama fadhilah ya yule anayewakusanya juu ya kusoma, basi katika hilo zipo dalili nyingi. Miongoni mwa dalili hizo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yule mwenye kujulisha katika kheri ni kama mtendaji wake.”[2]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Napaa kwa Allaah! Allaah kumwongoza kupitia wewe mtu mmoja ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”[3]
Hadiyth juu ya mada hii ni nyingi na zenye kutambulika. Isitoshe Allaah (Ta´ala) amesema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ
“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah.”[4]
Hapana shaka katika ukubwa wa malipo ya anayejitahidi katika hilo.
[1] ad-Daarimiy (3367).
[2] at-Tirmidhiy (2670), ambaye amesema kuwa ni ngeni kupitia njia hii. Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2670).
[3] al-Bukhaariy (309) na Muslim (405).
[4] 05:02
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 64-65
- Imechapishwa: 23/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 64-65
Imechapishwa: 23/11/2026
https://firqatunnajia.com/61-kisomo-cha-pamoja-kutoka-kwa-salaf/