60. Siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli cha ´Arshi

57 – al-´Irbaadh bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anh ) amesimulia kuwa Mtume (Swallâ Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) atasema: ”Wenye kupendana kwa ajili ya utukufu Wangu watakuwa chini ya kivuli cha ´Arshi Yangu – siku ambayo hakuna kivuli kingine isipokuwa kivuli Changu.”[1]

[1] Ahmad (4/128). al-Mundhiriy amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni nzuri.” (at-Targhiyb wat-Tarhiyb (4/48))

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy