Baadhi ya watambuzi walikuwa wamesema:
”Lau wafalme na watoto wa wafalme wangelijua yale tuliyomo, basi wangelipigana nasi juu yake kwa mapanga.
Mwingine amesema:
”Masikini watu wa dunia. Wametoka humo na hawakuonja kitu kitamu zaidi ndani yake.” Akaulizwa: ”Ni nini kitamu zaidi ndani yake?” Akasema: ”Mapenzi ya Allaah (Ta´ala), kumjua Yeye na kumtaja Yeye.”
Kuna mwingine wa tatu amesema:
”Hakika hupitia moyoni nyakati ambazo mtu hucheza kwa furaha.”
Kuna mwingine wa nne amesema:
”Hakika hunipitia nyakati ambapo hujiambia: ”Ikiwa watu wa Peponi wamo katika mfano wa haya, basi hakika wao wamo katika maisha mazuri.”
Kumpenda Allaah (Ta´ala), kumjua, kumtaja daima, kutulizana Kwake, kumtegemea na kumtegemea Yeye peke Yake kwa upendo, khofu, matumaini, utegemezi na matendo kwa namna ya kwamba Yeye peke Yake ndiye anayetawala mawazo ya mja, nia zake na matakwa yake – hiyo ndio Pepo na neema ya ulimwengu isiyofanana na neema yoyote ile. Aidha hiyo ndio burudani ya macho ya wanaopenda na uhai wa watambuzi. Macho ya watu hupata burudani kwa kiwango cha burudani ya macho yao kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo basi yule mwenye kupata burudani ya jicho lake kwa Allaah, basi kila jicho hupata burudani kupitia yeye. Na yule ambaye jicho lake halipati burudani kwa Allaah, basi nafsi yake hukatika kwa huzuni juu ya dunia. Hili halithibiti isipokuwa kwa mwenye moyo hai. Ama mwenye moyo uliokufa, basi atahisi ugeni kwa haya na kwa hivyo jifariji kwa kutokuwepo kwake kadiri uwezavyo, kwani kinachokusumbua si kutokuwepo kwake, bali ni kuwepo kwake mbele yako. Basi ukipewe majaribio naye basi mpe mgongo wako, mwache kwa moyo wako na jitenge naye kwa siri yako. Usijishughulishe naye ukapuuzia yaliyo bora kwako.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 110-111
- Imechapishwa: 21/08/2025
Baadhi ya watambuzi walikuwa wamesema:
”Lau wafalme na watoto wa wafalme wangelijua yale tuliyomo, basi wangelipigana nasi juu yake kwa mapanga.
Mwingine amesema:
”Masikini watu wa dunia. Wametoka humo na hawakuonja kitu kitamu zaidi ndani yake.” Akaulizwa: ”Ni nini kitamu zaidi ndani yake?” Akasema: ”Mapenzi ya Allaah (Ta´ala), kumjua Yeye na kumtaja Yeye.”
Kuna mwingine wa tatu amesema:
”Hakika hupitia moyoni nyakati ambazo mtu hucheza kwa furaha.”
Kuna mwingine wa nne amesema:
”Hakika hunipitia nyakati ambapo hujiambia: ”Ikiwa watu wa Peponi wamo katika mfano wa haya, basi hakika wao wamo katika maisha mazuri.”
Kumpenda Allaah (Ta´ala), kumjua, kumtaja daima, kutulizana Kwake, kumtegemea na kumtegemea Yeye peke Yake kwa upendo, khofu, matumaini, utegemezi na matendo kwa namna ya kwamba Yeye peke Yake ndiye anayetawala mawazo ya mja, nia zake na matakwa yake – hiyo ndio Pepo na neema ya ulimwengu isiyofanana na neema yoyote ile. Aidha hiyo ndio burudani ya macho ya wanaopenda na uhai wa watambuzi. Macho ya watu hupata burudani kwa kiwango cha burudani ya macho yao kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo basi yule mwenye kupata burudani ya jicho lake kwa Allaah, basi kila jicho hupata burudani kupitia yeye. Na yule ambaye jicho lake halipati burudani kwa Allaah, basi nafsi yake hukatika kwa huzuni juu ya dunia. Hili halithibiti isipokuwa kwa mwenye moyo hai. Ama mwenye moyo uliokufa, basi atahisi ugeni kwa haya na kwa hivyo jifariji kwa kutokuwepo kwake kadiri uwezavyo, kwani kinachokusumbua si kutokuwepo kwake, bali ni kuwepo kwake mbele yako. Basi ukipewe majaribio naye basi mpe mgongo wako, mwache kwa moyo wako na jitenge naye kwa siri yako. Usijishughulishe naye ukapuuzia yaliyo bora kwako.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 110-111
Imechapishwa: 21/08/2025
https://firqatunnajia.com/60-pepo-ya-duniani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket