60. Du´aa wakati mtu anapoyatembelea au kupita karibu na makaburi

146 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoka mwishoni mwa usiku kwenda al-Baqiy´ na akisema:

السَّلامُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ ، وَأَتَاكُمْ مَا تُوعَدُونَ، غَداً مُؤَجَّلُونَ، وَإِنَّا إِنْ شاءَ اللَّهُ بِكُمْ لاحِقُونَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِأَهْلِ بَقِيعِ الغَرْقَدِ

“Amani ya Allaah iwe juu yenu, wakazi waumini. Mmefikiwa na kile mlichoahidiwa. Ahadi yetu kukutana ni Kesho. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Ee Allaah! Wasamehe watu wa al-Baqiy´ al-Gharqad.”[1]

Ameipokea Muslim.

147 – Sulaymaan bin Burdaydah, kutoka kwa baba yake aliyesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwafunza wanapotoka kwenda makaburini. Alikuwa msemaji wao anasema:

السَّلَامُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الدِّيَارِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِينَ، وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ لَلَاحِقُونَ، أَسْأَلُ اللَّهَ لَنَا وَلَكُمُ الْعَافِيَةَ

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya.”[2]

Ameipokea Muslim.

Imekuja katika tamko jengine:

الاحقون

“… tutaungana na nyinyi.”[3]

MAELEZO

Katika Hadiyth hizi mbili kuna uwekwaji Shari´ah wa kuwatolea salamu watu wa makaburini na kuwaombea du´aa pindi mtu anapopita karibu na makaburi na ayaite kwa jina makaburi hayo aliyosimama karibu nayo. Akiacha kuyataja kwa jina haidhuru kitu kwa sababu du´aa imefika.

[1] Muslim (974).

[2] Muslim (975).

[3] Muslim (249).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 139
  • Imechapishwa: 15/11/2025