56 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameelea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (Ta´ala) atasema: ”Wako wapi wenye kupenda kwa ajili ya utukufu Wangu? Leo nitawafunika chini ya kivuli cha ´Arshi Yang – siku ambayo hakuna kivuli kingine isipokuwa kivuli Changu.”[1]

Kumepokelewa mapokezi mengi mno kuhusu kivuli cha ´Arshi.

[1] Swahiyh. Ameipokea Ahmad (2/338, 370 na 523) kupitia kwa Fulayh, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Ma´mar Abu Tiwaalah, kutoka kwa Sa´iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah. Kupitia njia hiyohiyo ameisimulia mtunzi katika asili, jambo ambalo ni la makosa. Kwa sababu Maalik ameipokea katika ”al-Muwattwa´” kupitia kwa Ibn Ma´mar, na yeye anaaminika zaidi ya mara elfu kuliko Fulayh. Kwa ajili hiyo Muslim ameipokea kupitia kwake. Vivyo hivyo ndivo alivofanya Ahmad (2/237 na 535) na ad-Daarimiy, uk. 371.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy