Hali hiyo ni kinyume cha watu wa furaha na mafanikio. Maisha yao ya duniani na baada ya kifo ni bora kabisa na Aakhira watapata malipo bora kabisa. Amesema (Ta´ala):
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً
“Yule mwenye kutenda mema katika wanamme au wanawake – ilihali ni muumini – basi Tutamhuisha maisha mazuri… ”
Bi maana ulimwenguni.
وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
“… na tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.”[1]
Bi maana Aakhirah. Amesema (Ta´ala):
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ
”Wale waliohajiri kwa ajili ya Allaah baada ya kudhulumiwa, kwa hakika tutawapa makazi mazuri duniani na ujira wa Aakhirah ni mkubwa zaidi – lau wangelikuwa wanajua!”[2]
وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى
”Muombeni Mola wenu msamaha kisha tubuni Kwake, atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalum uliokadiriwa… ”[3]
Bi maana ulimwenguni.
وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ
”… na Atampa kila mfanya mema kutoka katika fadhilah Zake.” [4]
Amesema (Ta´ala):
قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ
”Sema kuwaambia waja Wangu ambao mmeamini: ”Mcheni Mola wenu! Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Ardhi ya Allaah ni pana. Hakika hapana vyenginevyo wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu.”[5]
Hizi ni sehemu nne ambapo Allaah (Ta´ala) ametaja kuwa anamlipa mwenye kufanya wema kwa malipo mawili: malipo ya duniani na malipo ya Aakhirah. Hapana shaka yoyote kwamba wema una malipo na maovu yana malipo duniani, hata kama haingekuwa isipokuwa tu malipo anayolipwa mwenye kufanya wema ya kufunguka kifua chake, kufarijika kwa moyo wake, furaha, ladha ya kuambatana na Mola wake (´Azza wa Jall), utiifu, kumtaja Kwake na neema ya roho kwa kumpenda Yeye yangetosha. Kumtaja Yeye na kufurahi kwa Mola wake (Subhaanahu wa Ta´ala) ni jambo kubwa zaidi kuliko furaha ya yule aliyekaribiana na mtawala mkarimu kwa mamlaka yake. Na kinyume chake kinaweza kusemwa juu ya kile anaadhibiwa kwacho mwenye kufanya uovu ikiwa ni pamoja na dhiki ya kifua, ugumu wa moyo, kutawanyika, giza, chuki, huzuni, mashaka na khofu. Hili ni jambo ambalo mwenye hisia hata kidogo na uhai hawezi kulishuka. Bali huzuni, mashaka, huzuni na dhiki ni adhabu za haraka, moto wa ulimwengu na Jahannam ya sasa.
[1] 16:97
[2] 16:41
[3] 11:03
[4] 11:3
[5] 39:10
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 107-108
- Imechapishwa: 19/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 107-108
Imechapishwa: 19/08/2025
https://firqatunnajia.com/58-malipo-yasiyoepukika-ya-ulimwenguni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket