Atakayemsahau Allaah, basi atamsahaulisha nafsi yake duniani na atamsahau katika adhabu siku ya Qiyaamah. Amesema (Ta´ala):
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ
”Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu. Atasema: “Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona?” Atasema: “Hivyo ndivyo zilikufikia Aayah Zetu ukazisahau na kadhaalika leo umesahauliwa.”[1]
Bi maana kwamba utasahaulika katika adhabu kama ulivyosahau Aayah Zangu, kwa namna ya kwamba hukuzikumbuka wala hukuzifanyia kazi.
Kuipa mgongo Dhikr Yangu kunajumuisha kuachana kwake na Dhikr aliyoteremsha, kwa maana yale aliyoyateremsha ndani ya Kitabu Chake, ambayo pia ndio iliyokusudiwa katika Aayah, lakini kumdhukuru Mola kupitia majina Yake, sifa Zake, amri Zake, neema Zake. Haya yote yanakuja kama matokeo ya kupuuza kwake Kitabu cha Mola wake (Ta´ala). Kwa sababu Dhikr ndani ya Aayah hiyo ni kitendo kinachofanywa na Allaah au ni majina ya aina ya Dhikr yenyewe. Maana yake ameacha Kitabu Changu kwa namna ya kwamba hakukisoma, hakukitafakari, hakukitendea kazi wala hakukifahamu. Basi maisha yake na hali yake haitakuwa isipokuwa ni maisha yenye dhiki, yenye mashaka na yenye mateso.
Dhiki maana yake ni taabu, shida na mabalaa. Maisha kuelezwa kuwa yenye dhiki ni aina ya kusisitiza. Maisha haya yamefasiriwa kuwa ni adhabu baada ya kifo. Sahihi ni kuwa yanajumuisha maisha yake duniani na hali yake baada ya kifo, kwani atakuwa katika dhiki katika dunia na Aakhirah ambapo atapata shida, taabu na dhiki, ilihali Aakhirah atasahauliwa ndani ya adhabu.
[1] 20:124-126
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 106-107
- Imechapishwa: 19/08/2025
Atakayemsahau Allaah, basi atamsahaulisha nafsi yake duniani na atamsahau katika adhabu siku ya Qiyaamah. Amesema (Ta´ala):
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ
”Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu. Atasema: “Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona?” Atasema: “Hivyo ndivyo zilikufikia Aayah Zetu ukazisahau na kadhaalika leo umesahauliwa.”[1]
Bi maana kwamba utasahaulika katika adhabu kama ulivyosahau Aayah Zangu, kwa namna ya kwamba hukuzikumbuka wala hukuzifanyia kazi.
Kuipa mgongo Dhikr Yangu kunajumuisha kuachana kwake na Dhikr aliyoteremsha, kwa maana yale aliyoyateremsha ndani ya Kitabu Chake, ambayo pia ndio iliyokusudiwa katika Aayah, lakini kumdhukuru Mola kupitia majina Yake, sifa Zake, amri Zake, neema Zake. Haya yote yanakuja kama matokeo ya kupuuza kwake Kitabu cha Mola wake (Ta´ala). Kwa sababu Dhikr ndani ya Aayah hiyo ni kitendo kinachofanywa na Allaah au ni majina ya aina ya Dhikr yenyewe. Maana yake ameacha Kitabu Changu kwa namna ya kwamba hakukisoma, hakukitafakari, hakukitendea kazi wala hakukifahamu. Basi maisha yake na hali yake haitakuwa isipokuwa ni maisha yenye dhiki, yenye mashaka na yenye mateso.
Dhiki maana yake ni taabu, shida na mabalaa. Maisha kuelezwa kuwa yenye dhiki ni aina ya kusisitiza. Maisha haya yamefasiriwa kuwa ni adhabu baada ya kifo. Sahihi ni kuwa yanajumuisha maisha yake duniani na hali yake baada ya kifo, kwani atakuwa katika dhiki katika dunia na Aakhirah ambapo atapata shida, taabu na dhiki, ilihali Aakhirah atasahauliwa ndani ya adhabu.
[1] 20:124-126
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 106-107
Imechapishwa: 19/08/2025
https://firqatunnajia.com/57-maisha-ya-dhiki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket