57. Hapa ndipo Allaah alikuwa juu ya mbingu

54 – Wengi katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ

”Kisha akalingana juu ya mbingu.”[1]

”Allaah (Ta´ala) ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji. Hakuumba kitu kabla ya maji. Alipotaka kuwaumba viumbe, alitoa moshi kutoka kwenye maji, baadaye wakapanda. Halafu maji yakakauka na akayafanya ardhi. Kisha akaipasua na kuzifanya kuwa ardhi saba… Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipomaliza kuumba anavyovitaka, akalingana juu ya ´Arshi.”[2]

Ameipokea Ibn Jarir katika ”Jaamiy´-ul-Bayaan” na al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”.

[1] 41:11

[2] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Ibn Khuzaymah vilevile ameipokea.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 105
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy