Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma du´aa mbalimbali na akibadilisha katika nguzo hii:
1-
سبحان ربي الأعلى
“Ametakasika Mola wangu, Aliye juu kabisa, kutokamana na mapungufu yote.”
Akisema hivo mara tatu[1].
Wakati mwingine akikariri hivo zaidi ya mara tatu[2]. Kuna usiku mmoja ambapo aliikariri mara nyingi mpaka Sujuud yake ilikuwa ndefu inakaribiana na kisomo chake ambacho alikuwa anasoma ndani yake Suurah tatu ndefu: al-Baqarah, an-Nisaa´ na Aal ´Imraan. Ndani yake kulikuwa du´aa na kuomba msamaha, kama ilivyotangulia katika swalah ya usiku.
2-
سبحان ربي الأعلى وَ بِحَمْدِهِ
“Ametakasika Mola wangu, Aliye juu kabisa, kutokamana na mapungufu yote na himdi zote ni Zake.”
Akisema hivo mara tatu[3].
3-
سُبُّوحٌ قُدُّوسٌ رَبُّ الْمَلائِكَةِ والرُّوح
“Umetakasika sana kutokamana na mapungufu na uchafu; Mola wa Malaika na roho!”[4]
4-
سبحانك اللهم ربنا و وبحمدك,اللهم اغفر لي
“Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote unastahiki Wewe. Ee Allaah! Nisamehe!”
Alikuwa akiisoma mara nyingi katika Rukuu´ na Sujuud yake na akiitendea kazi Qur-aan[5].
5-
اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آَمَنْتُ وَلَكَ أَسْلَمْتُ سَجَدَ وَجْهِي لِلَّذِي خَلَقَهُ وَصَوَّرَهُ وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ تَبَارَكَ الله أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ
Ee Allaah! Kwako Wewe nimesujudu. Wewe nimekuamini. Kwako Wewe nimejisalimisha. Usikizi wangu, uoni wangu, ubongo wangu, mifupa yangu na mishipa yangu vimenyenyekea Kwako. Ametukuka Allaah, mbora kabisa wa waumbaji.”[6]
6-
اللهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ دِقَّهُ وَجِلَّهُ وأَوَّلهُ وآخِرَهُ وَعَلانِيَتَهُ وَسِرَّهُ
“Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri.”[7]
7-
سَجَدَ لَكَ سَوَاديِ وَخيَالِي ، وَآمَنَ بِكَ فُؤَادِي ، هَذِهِ يَدِي وَمَا جَنَيْتُ عَلَى نَفْسِي
“Utu na kivuli changu vimekusujudia Wangu. Moyo wangu umekuamini. Nakiri neema Zako kwangu. Huu hapa mkono wangu na yale yote niliyochuma dhidi ya nafsi yangu mwenyewe.”[8]
8-
سُبْحَانَ ذِي الجبروتِ وَالملكوتِ والْكِبْرِياءِ والْعَظَمة
“Ametakasika kutokamana na mapungufu Mwenye utawala, ufalme, ukubwa na utukufu.”[9]
9-
سبحانك اللهم و بحمدك. لا إله إلا أنت
“Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote unastahiki Wewe. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”[10]
10-
اللهم اغْفِرْ لِي ما أَسْرَرْتُ وَ ما أَعْلَنْتُ
“Ee Allaah! Nisamehe yale ninayoyaficha na yale ninayoyaonyesha.”[11]
11-
اللهمَّ !اجعلْ لي في قلبي نورًا ، وفي لساني نورًا ، وفي سمعي نورًا ، وفي بصري نورًا ، ومن فوقي نورًا ، ومن تحتي نورًا ، وعن يميني نورًا ، وعن شمالي نورًا ، ومن بين يديَّ نورًا ، ومن خلفي نورًا ، واجعلْ في نفسي نورًا ، وأَعظِمْ لي
“Ee Allaah! Niweke nuru katika moyo wangu, katika ulimi wangu nuru, katika usikizi wangu nuru, katika uoni wangu nuru, juu yangu nuru, chini yangu nuru, upande wangu wa kulia nuru, upande wangu wa kushoto nuru, mbele yangu nuru, nyuma yangu nuru, niweke nuru katika nafsi yangu na nikuzie nuru.”[12]
12-
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعوذُ برِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ وَبِمُعَافَاتِكَ منْ عُقُوبَتِكَ وَأَعُوذُ بِكَ منك لاَ أُحْصي ثَنَاءً عَلَيْكَ. أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ على نَفْسِكَ
“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokamana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokamana na adhabu Zako. Najilinda Kwako unihifadhi na Wewe. Siwezi kuzidhibiti sifa Zako. Wewe ni vile Mwenyewe ulivyojisifu.”[13]
[1] Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, ad-Daaraqutwniy, at-Twahaawiy, al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kupitia Maswahabah saba.
[2] Mtu amepata kufikia kupitia Hadiyth zilizoweka wazi ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumia muda mrefu sawa katika kisimamo chake, Rukuu´ na Sujuud, kama itavyokuja katika mlango unaofuata.
[3] Swahiyh. Abu Daawuud, ad-Daaraqutwniy, Ahmad, at-Twabaraaniy na al-Bayhaqiy.
[4] Muslim na Abu ´Awaanah.
[5] al-Bukhaariy na Muslim. Du´aa hii inaweza pia kusomwa katika Rukuu´.
[6] Muslim, Abu ´Awaanah, at-Twahaawiy na ad-Daaraqutwniy.
[7] Muslim na Abu ´Awaanah.
[8] Ibn Naswr, al-Bazzaar na al-Haakim aliyeisahihisha lakini akaraddiwa na adh-Dhahabiy. Lakini hata hivyo ina mapokezi yanayoitia nguvu niliyoyataja katika kile kitabu asili.
[9] Abu Daawuud na an-Nasaa’iy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.
[10] Muslim, Abu ´Awaanah, an-Nasaa’iy na Ibn Naswr.
[11] Ibn Abiy Shaybah (1/112/62) na an-Nasaa’iy. al-Haakim ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
[12] Muslim, Abu ´Awaanah na Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (1/112) na (2/106/12).
[13] Muslim, Abu ´Awaanah na Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (1/112) na (2/106/12).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 126-127
- Imechapishwa: 04/08/2017

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 126-127
Imechapishwa: 04/08/2017
https://firqatunnajia.com/57-adhkaar-za-kwenye-sujuud/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)