54. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah – nyepesi kabisa

Yaliyosemwa na ar-Raaziy ni hoja juu ya ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah. Hakupata kitu kilicho salama na cha uchaji zaidi kama njia yao, hakupata dalili na majulisho sahihi zaidi kama majulisho ya Qur-aan. Katika kuthibitisha sifa unasoma na kuamini:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

Katika kukanusha kufanana unasoma Aayah:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Unamthibitishia Allaah sifa kamilifu ambazo amejithibitishia nazo Mwenyewe na ambazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemthibitishia nazo juu ya uhakika wake, na sambamba na hayo unamkanushia Allaah kufanana ambako hawa wamedhania kuwa ambaye anamthibitishia Allaah sifa basi anakuwa mwenye kufananisha. Hakuna mgongano kati ya:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

na:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[2]

Yule mwenye kuyajaribu haya basi ataitambua haki na atasalimika kutokana na batili ambayo wametumbukia ndani yake wale wanaokanusha sifa za Allaah.

[1] 42:11

[2] 42:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 12/08/2024