53. Washirikina waliwaabudu waungu wengine kwa ajili ya uombezi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwambie pia: “Washirikina ambao waliteremshiwa Qur-aan, je walikuwa wakiabudu Malaika, watu wema, al-Laat na wengineo?” Hana budi kusema: “Ndio”. Hivyo mwambie: “Je, ´ibaadah yao [kuwaabudu] kwao ilikuwa ni katika du´aa peke yake, kuchinja, kutafuta kinga kwao na mfano wa hayo?” La sivyo walikuwa wakikiri kuwa ni waja Wake, walio chini ya uwezo Wake na kwamba Allaah ndiye Mwenye kuyaendesha mambo yote, lakini waliwaomba na kuwaelekea kwao kwa sababu wana jaha na [wanatafuta] uombezi – na hili ni jambo liko wazi sana.”

MAELEZO

Hapa mtunzi (Rahimahu Allaah) anaenda katika malazimisho mengine ambayo nimeyaashiria punde. Anamuuliza mpinzani kama washirikina walikuwa wanaabudu Malaika, watu wema, al-Laat na wengineo. Hana budi kusema: “Ndio.” Halafu amuulize swali lingine na kumwambia: “Je, ´ibaadah yao haikuwa kwa kitu kingine zaidi ya du´aa, kuchinja, kuomba kinga na mfano wa hayo?” Walikuwa wakijua kuwa wao ni waja wa Allaah, walio chini ya uwezo Wake na kwamba Allaah ndiye ambaye anayaendesha mambo yote. Hata hivyo waliwaabudu na kuwaelekea kwa sababu walikuwa na haja na kuomba uombezi, kama tulivyotangulia kusema, na haya ndio yaleyale ambayo wametumbukia ndani yake wapinzani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 68
  • Imechapishwa: 24/11/2023