82 – Na akitaka kuwaadhibu basi atawaadhibu Motoni kutokana na uadilifu Wake. Kisha atawatoa humo kwa rehema Zake na kwa uombezi wa waja Wake watifiu watakaowaombea. Kisha atawaingiza katika Pepo Yake. Hivyo ni kwa sababu Allaah amedhamini kuwalinda wale wenye kumtambua. Hatowachukulia duniani na Aakhirah kuwa kama wale waliomkanusha, waliokosa mwongozo Wake na hawakupata ulinzi Wake. Ee Allaah! Wewe unayelinda Uislamu na waislamu! Tuthibitishe juu ya Uislamu mpaka pale tutapokutana Nawe tukiwa nao!

MAELEZO

Hii ni du´aa iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imetajwa katika ”as-Swahiyhah” (1823), kama nilivyotaja katika ukaguzi wangu ”Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah”. Hata hivyo ni kosa la uchapaji, badala yake namba ikaonyesha (1833). Ndio maana ikasahihishwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 74
  • Imechapishwa: 07/10/2024