1 – Nasaba yake:
Alikuwa ni Shaykh-ul-Islaam, hoja ya ummah, imamu wa Madiynah Abu ´Abdillaah Maalik bin Anas bin Maalik bin Abiy ´Aamir bin ´Amr bin al-Haarith bin Ghayman bin Khuthayl bin ´Amr al-Haarith, ambaye alikuwa Dhuu Aswbah bin ´Afw bin Maalik bin Zayd bin Shaddaad bin Zur´ah, anaitwa pia Hamiyr-ul-Aswghar, al-Humayriy al-Aswbahiy al-Madaniy. Walifungamana na Banuu Tamiym kutoka Quraysh. Walikuwa na mafungamano na ´Uthmaan, ndugu yake Twalhah bin ´Ubaydillaah – mmoja katika wale Maswahabah kumi waliobashiriwa Pepo.
2 – Kuzaliwa kwake:
adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Maoni sahihi ni kwamba Maalik alizaliwa mwaka wa 93, mwaka uleule ambao alikufa Anas, ambaye ni mfanya kazi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Akakulia juu ya uangalizi, anasa na kujipamba.”
3 – Makuzi yake na kutafuta kwake elimu:
Maalik alianza kutafuta elimu alipokuwa na umri wa zaidi ya miaka kumi na kitu. Alikuwa na ustahiki wa kutoa fatwa na akatoa fatwa akiwa na miaka ishirini na moja. Wengi wamehadithia kutoka kwake akiwa bado ni kijana chipukizi na wengine wakisafiri kumwendea kutoka pembe zote za ulimwengu mwishoni mwa ukhaliyfah wa Abu Ja’far al-Mansuur na hata baada ya hapo. Wakati wa ukhaliyfah wa ar-Rashiyd umati wa watu walikuwa wakimkusanyikia mpaka alipokufa.
4 – Waalimu wake:
Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) alikuwa kijana mdogo wakati alipoanza kutafuta elimu mara baada ya kifo cha al-Qaasim na Saalim. Badala yake akasoma kwa Naafiy’, Sa’iyd al-Maqburiy, ´Aamir bin ´Abdillaah bin az-Zubayr, Ibn-ul-Munkadir, az-Zuhriy, ´Abdullaah bin Diynaar na wengineo. adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) ameorodhesha walimu wa Imaam Maalik ambao amepokea kutoka kwao katika “al-Muwattwa'” kwa mpangilio wa kialfabeti na baadhi ya wale aliyosimulia kutoka kwao.
5 – Wanafunzi wake:
adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Nimeandika majina ya waliosimulia kutoka kwake kwenye juzuu kubwa. Wanakaribia wasimulizi 1,400. Hebu wacha tutaje wale maarufu zaidi. Miongoni mwa waalimu wake, ambao pia wamehadithia kutoka kwake, ni ami yake Abu Suhayl, Yahyaa bin Abiy Kathiyr, az-Zuhriy, Yahyaa bin Sa’iyd, Zayd bin al-Haad, Zayd bin Unaysah na ´Amr bin Muhammad bin Zayd. Miongoni mwa rika lake ni pamoja na Ma’mar, Ibn Jurayj, Abu Haniyfah, ‘Amr bin al-Haarith, al-Awzaa’iy, Shubah, ath-Thawriy…”
6 – Tungo zake
Miongoni mwa tungo zake (Rahimahu Allaah) ni pamoja na:
1 – al-Muwattwa’.
2 – Kijitabu kuhusu makadirio akimwandikia Ibn Wahb.
3 – Kijitabu kuhusu nyota na matuo ya mwezi.
4 – Kijitabu kuhusu hukumu.
5 – Kijitabu kwenda kwa Abu Ghassaan bin Mutwarrif.
6 – Sehemu katika tafsiri ya Qur-aan.
Kwa kuongezea maswahiba wake wakubwa wamenakili maswali, maoni na faida kiasi kikubwa.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 13-15
- Imechapishwa: 26/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 13-15
Imechapishwa: 26/11/2025
https://firqatunnajia.com/5-nasaba-makuzi-na-kusoma-kwa-imaam-maalik/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket