Unyenyekevu moyoni unatofautiana kwa kutegemea na kule kumtambua yule unayemnyenyekea pamoja na uzoefu wake wa yale yanayopelekea unyenyekevu.
Yule ambaye anajinyenyekeza kwa sababu ya kuhisi ukaribu wenye nguvu wa Allaah na mja Wake na anajua siri Zake, anamuonea haya Allaah (Ta’ala) na anamchunga katika hali zake zote za kutikisika na zisizotikisika.
Anayejinyenyekeza kwa sababu anajua kuwa Yeye ni mkamilifu na mzuri, anampenda sana na anatamani sana kukutana Naye na kumuona.
Anayejinyenyekeza kwa sababu anajua kuwa anaadhibu, analipiza kisasi na anaadhibu vikali, humwogopa.
Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anazitia nguvu nyoyo zenye kumnyenyekea kwa ajili Yake. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anamkurubia yule anayemuomba ndani ya swalah na kuuweka uso wake wakati amesujudu. Kadhalika Yeye anawakurubia waja Wake wanaomwomba, kumuuliza, kumuomba msamaha kutokana na madhambi yao katika nyakati za usiku wa mwisho. Anawaitikia du´aa zao na kuwaitikia maombi yao. Hakuna kitu kikubwa kinachotia nguvu moyo wa mja uliyovunjika kama ukaribu na kuitikia maombi. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amepokea katika “Kitaab-uz-Zuhd” kwamba ´Imraan al-Qaswiyr amesema:
“Muusa (‘alayhis-Salaam) alisema: “Ee Mola, nitakutafuta kwa bidii wapi?” Akasema: “Nitafuteni kwa bidii kwa wale ambao nyoyo zao zimevunjika kwa ajili Yangu. Kwani hakika Mimi huwakurubia kila siku paa moja – vinginevyo wangelivunjika.”
Ibraahiym al-Junayd (Rahimahu Allaah) amepokea katika “Kitaab-ul-Mahabbah” ya kwamba Ja’far bin Sulayman amemsikia Maalik bin Diynaar akisema:
“Muusa (‘alayhis-Salaam) alisema: “Ee Mola, nitakutafuta kwa bidii wapi?” Allaah (Ta´ala) akamteremshia wahy: ”Ee Muusa! Nitafuteni kwa bidii kwa wale ambao nyoyo zao zimevunjika kwa ajili Yangu. Kwani hakika Mimi huwakurubia kila mchana na usiku paa moja – vinginevyo wangelivunjika.”
Ja’far alisema: “Nilimuuliza Maalik bin Diynaar ni namna gani nyoyo zao huvunjika. Akajibu: “Nilimuuliza vivyo hivyo mtu aliyenisomea kwenye kitabu. Akasema kwamba alimuuliza yule mtu ambaye alimuuliza ´Abdullaah bin Salaam ni namna gani nyoyo zao huvunjika, ambapo akasema: “Nyoyo zao zinavunjika kwa sababu ya kumpenda Allaah (´Azza wa Jall).”
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 37-41
- Imechapishwa: 24/11/2025

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 37-41
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/5-aina-mbalimbali-ya-unyenyekevu/