Abu Sa´iyd amesimulia:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa: “Ni nani miongoni mwa waja aliye bora na mwenye daraja ya juu zaidi kwa Allaah siku ya Qiyaamah?” Akasema: “Wale wanaomtaja Allaah sana.” Wakauliza: “Ee Mtume wa Allaah, vipi mpiganaji jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema: “Hata akipigana kwa upanga wake dhidi ya makafiri na washirikina mpaka upasuke na uchanganyike na damu, bado yule anayemtaja Allaah (Ta´ala) ni bora zaidi kidaraja kuliko yeye.”[1]
Ameipokea at-Tirmidhiy.
Abu Muusa amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mfano wa anayemtaja Mola wake na asiyemtaja Mola wake ni mfano wa aliye hai na aliyekufa.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amesema: “Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania na Mimi ni pamoja Naye anaponitaja. Akinitaja kwenye nafsi yake Nami namtaja kwenye nafsi Yangu, akinitaja katika kundi, Nami namtaja katika kundi ambalo ni bora kuliko wao, akijikurubisha Kwangu paa moja Nami najikurubisha kwake dhiraa, akijikurubisha Kwangu dhiraa Nami najikurubisha kwake kwa kiasi cha kunyoosha mkono hadi kati ya kifuwa na akinijia kwa mwendo mdogo basi Mimi nitamjia kwa kuchapuka.”[3]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Anas amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mkipita kwenye bustani za Peponi, basi lisheni.” Wakauliza: “Ee Mtume wa Allaah, ni nini bustani za Peponi?” Akasema: “Vikao vya kumtaja Allaah.”[4]
Ameipokea at-Tirmidhiy.
Yeye pia amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika mja Wangu wa kweli ni yule anayenitaja wakati anapomuona adui yake sawa na uwazi wa jicho lake.”[5]
Hadiyth hii ni fasili ya hoja na utenganisho kati ya mwenye kumtaja na mpiganaji jihaad. Kwani mwenye kumtaja Allaah ambaye pia ni mpiganaji jihaad ni bora kuliko mwenye kumtaja Allaah bila jihaad na mpiganaji jihaad asiyemtaja Allaah. Mwenye kumtaja Allaah bila jihaad ni bora kuliko mpiganaji jihaad asiyemtaja Allaah. Basi bora ya wenye kumtaja Allaah ni wapiganaji wa jihaad, na bora ya wapiganaji wa jihaad ni wale wanaomtaja Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
”Enyi walioamini! Mtapokutana na kikosi, basi simameni imara na mtajeni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu.”[6]
Amewaamrisha kufanya Dhikr kwa wingi na jihaad ili kufikia mafanikio. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا
“Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru!”[7]
وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ
“Wanaume wanaomdhukuru Allaah kwa wingi na wanawake [wanaofanya hivo].”[8]
[1] Ahmad (4/190) na at-Tirmidhiy (3376), aliyesema kuwa Hadiyth ni ngeni. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (3376).
[2] al-Bukhaariy (6407).
[3] al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675).
[4] Ahmad (4/387) na at-Tirmidhiy (3510), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni. Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3510).
[5] at-Tirmidhiy (3580), aliyesema kuwa Hadiyth ni ngeni. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (3580).
[6] 8:45
[7] 33:41
[8] 33:35
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 86-89
- Imechapishwa: 17/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 86-89
Imechapishwa: 17/08/2025
https://firqatunnajia.com/49-tofauti-ya-aliye-hai-na-maiti/