Kwa kuongezea ni kwamba maneno ya Rabiy’ah na Maalik yamefanana kabisa na ya Abu Ja’far at-Tirmidhiy (aliyefariki mwaka 295) wakati alipoulizwa kuhusu Kushuka. al-Khawiyb al-Baghdaadiy amesema: al-Hasan bin Abiy Twaalib amenihadithia: Abul-Hasan Mansuur bin Muhammad bin Mansuur al-Qazzaaz ametueleza: Nimemsikia Abut-Twayyib Ahmad bin ´Uthmaan as-Simsaar, baba yake Abu Hafsw bin Shaahiyn, akisema:
“Nilikuwa nimehudhuria kwa Abu Ja’far at-Tirmidhiy wakati mtu mmoja alipomuuliza kuhusu Hadith ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Allaah (Ta’ala) hushuka kwenye mbingu ya chini kabisa…”
Akasema: ”Kushuka kunakuweje ikiwa kunaacha ujuu?” Abu Ja’far at-Tirmidhiy akajibu: “Kushuka kunatambulika na namna haijulikani. Ni wajibu kuamini hilo na kuulizia hilo ni Bid´ah.”[1]
adh-Dhahabiy ameitaja katika “al-‘Uluww” na al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) akasema:
“Wasimulizi wa cheni ya wapokezi woete ni madhubuti.”[2]
adh-Dhahabiy akayatolea masimulizi haya maelezo na kusema:
“Mwanachuoni wa wakati wake huko Baghdaad amesema kweli. Kuna maana gani kuuliza juu ya Kushuka? Kufeli. Maswali huulizwa juu ya maneno ya kigeni katika lugha, vinginevyo, ushukaji, maneno, kusikia, kuona, ujuzi na kulingana juu na ni maneno yaliyo wazi kwa msikilizaji. Ikiwa Yeye, ambaye hakuna yeyote anayefanana naye, anasifiwa kwayo, basi itambulike kuwa wasifu ni wenye kumwandana yule msifiwa. Namna yake ni kitu kisichotambulika kwa mwanadamu. at-Tirmidhiy huu alikuwa ni mwenye elimu ya kina na miongoni mwa waja wanaomcha Allaah. Alifariki mwaka wa 295.”[3]
[1] Taariykh Baghdaad (1/365).
[2] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 232.
[3] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 231.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 71
- Imechapishwa: 12/12/2025
Kwa kuongezea ni kwamba maneno ya Rabiy’ah na Maalik yamefanana kabisa na ya Abu Ja’far at-Tirmidhiy (aliyefariki mwaka 295) wakati alipoulizwa kuhusu Kushuka. al-Khawiyb al-Baghdaadiy amesema: al-Hasan bin Abiy Twaalib amenihadithia: Abul-Hasan Mansuur bin Muhammad bin Mansuur al-Qazzaaz ametueleza: Nimemsikia Abut-Twayyib Ahmad bin ´Uthmaan as-Simsaar, baba yake Abu Hafsw bin Shaahiyn, akisema:
“Nilikuwa nimehudhuria kwa Abu Ja’far at-Tirmidhiy wakati mtu mmoja alipomuuliza kuhusu Hadith ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Allaah (Ta’ala) hushuka kwenye mbingu ya chini kabisa…”
Akasema: ”Kushuka kunakuweje ikiwa kunaacha ujuu?” Abu Ja’far at-Tirmidhiy akajibu: “Kushuka kunatambulika na namna haijulikani. Ni wajibu kuamini hilo na kuulizia hilo ni Bid´ah.”[1]
adh-Dhahabiy ameitaja katika “al-‘Uluww” na al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) akasema:
“Wasimulizi wa cheni ya wapokezi woete ni madhubuti.”[2]
adh-Dhahabiy akayatolea masimulizi haya maelezo na kusema:
“Mwanachuoni wa wakati wake huko Baghdaad amesema kweli. Kuna maana gani kuuliza juu ya Kushuka? Kufeli. Maswali huulizwa juu ya maneno ya kigeni katika lugha, vinginevyo, ushukaji, maneno, kusikia, kuona, ujuzi na kulingana juu na ni maneno yaliyo wazi kwa msikilizaji. Ikiwa Yeye, ambaye hakuna yeyote anayefanana naye, anasifiwa kwayo, basi itambulike kuwa wasifu ni wenye kumwandana yule msifiwa. Namna yake ni kitu kisichotambulika kwa mwanadamu. at-Tirmidhiy huu alikuwa ni mwenye elimu ya kina na miongoni mwa waja wanaomcha Allaah. Alifariki mwaka wa 295.”[3]
[1] Taariykh Baghdaad (1/365).
[2] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 232.
[3] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 231.
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 71
Imechapishwa: 12/12/2025
https://firqatunnajia.com/49-tamko-la-abu-jafar-at-tirmidhiy-la-masimulizi-ya-maalik/