Amesema (Rahimahu Allaah):

“… akawategemea… “

Waabudu makaburi wanawategemea wafu. Miongoni mwao wako wanaomwambia maiti: “Ee fulani! Mimi nakutegemea wewe”. Hawamtegemei Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wala hukuti wakimtaja Allaah katika ndimi zao. Isipokuwa wao daima wameshikamana na yule wanayemuabudu badala ya Allaah na wanamtegemea. Kutegemea ni aina kubwa kabisa ya ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

”Kwa Allaah pekee tegemeeni ikiwa nyinyi ni waumini.” (al-Maaidah 05:23)

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

”Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea.” (al-Anfaal 08:02)

Bi maana miongoni mwa sifa zao ni kwamba wanamtegemea Mola wao na si mwingine. Ametangulizwa Allaah mbele kuonyesha kukomeka:

وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

“… na kwa Mola wao wanategemea.”

Hakusema kwamba wanamtegemea Mola wao. Bali amesema:

وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

“… na kwa Mola wao wanategemea.”

Ametangulizwa Allaah mbele kuonyesha kukomeka. Ni kama mfano wa maneno Yake (Ta´ala):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

“Wewe pekee tunakuabudu.“ (al-Faatihah 01:05)

Bi maana hakuna mwingine tunayemuabudu zaidi Yako. Hili ni lenye kugonga zaidi kuliko kusema:

نعبدك

“Tunakuabudu.”

Kwa sababu kusema hivi hakufidishi ukomekaji. Lakini:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

“Wewe pekee tunakuabudu.“

kunafidisha ukomekaji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 04/09/2018