Tulikwishatangulia katika kipengele kilichotangulia kuhimiza kutafakari na kubainisha nafasi yake na namna Salaf walivyokuwa wakiathirika. Tumesimuliwa kwamba Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikariri Aayah moja akiirudia mpaka asubuhi, nayo ni:
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ
“Ukiwaadhibu, basi hao ni waja Wako.”[1]
Ameipokea an-Nasaaiy na Ibn Maajah.
Tumesimuliwa pia kwamba Tamiym ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) alirudia Aayah ifuatayo mpaka asubuhi:
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ
“Je, wanadhania wale waliochuma mabaya Tuwafanye wawe sawa na wale walioamini na wakatenda mema na pia sawasawa uhai wao na kufa kwao? – uovu ulioje wanaouhukumu!”[2]
´Ubaadah bin Hamzah amesema:
”Niliingia kwa Asmaa´ (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alikuwa akisoma:
فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ
“Basi Allaah akatuneemesha na akatuokoa na adhabu ya Moto unaobabua.”[3]
Akisimama hapo, akianza kuirudia na kuomba du´aa. Nikaona muda umekuwa mrefu kwangu, nikaenda sokoni, nikamaliza haja yangu, kisha nikarudi, naye bado anairudia na kuomba du´aa.
Kisa hiki kimesumuliwa pia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).
Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akirudia Aayah:
وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا
“Sema: ”Mola wangu! Nizidishie elimu.”[4]
Sa´iyd bin Jubayr alikuwa akirudia Aayah:
وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ
”Iogopeni Siku mtakayorejeshwa kwa Allaah!”[5]
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِالْكِتَابِ وَبِمَا أَرْسَلْنَا بِهِ رُسُلَنَا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ إِذِ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ
”Wale waliokadhibisha Kitabu na yale tuliyowatuma nayo Mitume Wetu, basi punde watakuja kujua; zitakapokuwa pingu shingoni mwao.”[6]
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ
“Ee mwanadamu! Nini kilichokughuri juu ya Mola wako mkarimu?”[7]
adh-Dhwahhaak alikuwa akirudia maneno Yake (Ta´ala) mpaka alfajiri:
لَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ النَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ
”Watawekewa kutoka juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka.”[8]
[1] 5:118 an-Nasaa’iy (1009) na Ibn Maajah (1350). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan an-Nasaa’iy” (1009).
[2]45:21
[3] 52:27
[4] 20:114
[5] 2:281
[6] 40:70-71
[7] 82:6
[8] 39:16
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 56
- Imechapishwa: 01/09/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 56
Imechapishwa: 01/09/2026
https://firqatunnajia.com/49-kukariri-aayah-moja-kwa-sababu-ya-mazingatio-2/