Shubuha ya tano: Washirikina wa mwanzo walikuwa wakiomba masanamu, wakiwaomba mashaytwaan na majini. Ama sisi tunawaomba watu wema. Vipi mtawafanya watu wema ni kama masanamu?
Tunasema: Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu! Je, nyinyi hamsomi Qur-aan? Je, washirikina wa mwanzo hawakuwa wakiomba uombezi kutoka kwa Malaika ambao ni waja wema na wakiwaomba uombezi Mitume baada ya kufa kwao? Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ
”Wanaabudu badala ya Allaah ambao hawawezi kuwadhuru na wala kuwanufaisha na huku wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (Yuunus 10:18)
Walikuwa wakiwaabudu Malaika, al-´Uzayr na al-Masiyh. Walikuwa wakiabudu watu wema. Washirikina kabla ya kuja Uislamu walikuwa ni wenye kutofautiana katika ´ibaadah zao. Miongoni mwao kulikuwa wanaoabudu masanamu, jua na mwezi, miti na mawe, Malaika, watu wema na mawalii. Yale waliyomo hii leo waabudu makaburi ni aina moja wapo katika shirki ya watu wa mwanzo ambao wanawaabudu Malaika, Manabii na watu wema:
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ
”Wale waliojichukulia badala Yake walinzi [na huku wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” Hakika Allaah atahukumu baina yao katika yale yote waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah hamwongoi aliye muongo, kafiri.” (az-Zumar 39:03)
Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya waabudu makaburi washirikina wa leo na wale waliotangulia. ´Ibaadah ya washirikina wa kale haikufupika kuyaabudu masaamu peke yake, kama mnavosema, wala haikufupika kuiabudu miti na mawe. Lakini wako ambao walikuwa wakiwaabudu waja wema kutokana na dalili ya Qur-aan. Allaah ametaja kwamba walikuwa wakiwaabudu Malaika na watu katika waja Wake. Amesema (Ta´ala):
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia… “ (al-Israa´ 17:57)
Ni dalili ioneshayo ya kwamba walikuwa wakiwaabudu waja wema ambao wao wenyewe wanatafuta kwa Mola wao njia kwa kumtii. Jambo hili liko wazi, lakini watu hawa wanajifanya hamnazo. Ni wajibu kwa mwanafunzi awe juu ya bayana katika mambo haya na khaswa khaswa walinganizi ambao wanajinasibisha kulingania kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwani watawaelekezea mfano wa shubuha hizi. Ni wajibu kwao wajifunze mambo haya na wayajue ili waweze kuwaraddi watu hawa wanaotatiza ambao wamewaangamiza watu kwa sababu ya shubuha zao.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 72-73
- Imechapishwa: 04/09/2018

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 72-73
Imechapishwa: 04/09/2018
https://firqatunnajia.com/48-shubuha-ya-tano-washirikina-wa-kale-walikuwa-wakiomba-masanamu-lakini-sisi-tunawaomba-waja-wema-na-majibu-juu-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)