Ibn Qudaamah amenukuu masimulizi yote haya matatu ya Umm Salamah, Rabiy´ah na Maalik na kusema:

“Maneno haya yamekaribiana maana na matamshi. Inawezekana Maalik na Rabiy´ah walifikiwa na khabari yale yaliyosemwa na Umm Salamah ambapo na wao wakawa wameyaiga kutokana na usahihi wake na uzuri wake na jengine ni kwa sababu alikuwa mmoja katika wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inawezekana vilevile Allaah (Ta´ala) aliwahidi katika usawa na akawapa ilham ya kuongea maneno ya kisawasawa kama alivyompa ilham Umm Salamah.”

Imekwishatangulia ya kwamba masimulizi ya Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) hayakuthibiti kutoka kwake. Kwa hivyo kumebaki mbadala wa pili, kwamba Allaah (Ta´ala) amewaongoza katika usawa na akawapa ilhamu kutamka maneno haya ya sawa. Pengine Maalik aliyasikia kutoka kwa mwalimu wake Rabiy´ah na hivyo akamwigiliza au kwamba hakuyasikia kutoka kwake lakini hata hivyo akamuwafikisha kwayo kama alivyowafikishwa mwalimu wake. adh-Dhahabiy ametaja katika “al-Arba’iyn fiy Swifaati Rabb-il-Aalamiyn”[1], ya kwamba masimulizi haya yamepokelewa pia kutoka kwa Wahb bin Munabbih, hata hivyo sikuyaona.

[1] al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn (9).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 70-71