Miongoni mwa watu wapo wanaotaka kulitumia vibaya upole wa Uislamu ambapo wakajiruhusu kufanya yaliyoharamishwa na kuacha yaliyo wajibu huku wakisema eti dini ni nyepesi. Ndio, hakika dini ni nyepesi, lakini hilo halimaanishi kwamba mtu ajivue katika hukumu zake na kufuata matamanio ya nafsi yake. Bali maana ya upole wa Uislamu ni kwamba humhamisha mja kutoka ´ibaadah nzito kwenda ´ibaadah nyepesi anayoimudu katika hali ya udhuru. Miongoni mwa hilo ni kuwahamisha wenye udhuru wa Kishari´ah kutoka kufunga kwa kutekeleza ndani ya Ramadhaan kwenda kufunga kwa kulipa katika mwezi mwingine pale udhuru wao unapondoka, au kuwahamisha kutoka kufunga kwenda kulisha iwapo hawawezi kulipa. Hivyo akawakusanyia utekelezaji wa wajibu pamoja na kuondoka kwa mashaka na dhiki. Basi sifa njema na fadhilah ni za Allaah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 45
- Imechapishwa: 19/03/2026
Miongoni mwa watu wapo wanaotaka kulitumia vibaya upole wa Uislamu ambapo wakajiruhusu kufanya yaliyoharamishwa na kuacha yaliyo wajibu huku wakisema eti dini ni nyepesi. Ndio, hakika dini ni nyepesi, lakini hilo halimaanishi kwamba mtu ajivue katika hukumu zake na kufuata matamanio ya nafsi yake. Bali maana ya upole wa Uislamu ni kwamba humhamisha mja kutoka ´ibaadah nzito kwenda ´ibaadah nyepesi anayoimudu katika hali ya udhuru. Miongoni mwa hilo ni kuwahamisha wenye udhuru wa Kishari´ah kutoka kufunga kwa kutekeleza ndani ya Ramadhaan kwenda kufunga kwa kulipa katika mwezi mwingine pale udhuru wao unapondoka, au kuwahamisha kutoka kufunga kwenda kulisha iwapo hawawezi kulipa. Hivyo akawakusanyia utekelezaji wa wajibu pamoja na kuondoka kwa mashaka na dhiki. Basi sifa njema na fadhilah ni za Allaah.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 45
Imechapishwa: 19/03/2026
https://firqatunnajia.com/48-maana-ya-kwamba-dini-ni-nyepesi/