48. Kursiy (الكرسي) ni mahali pa kuwekea miguu miwili

45 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Kursiy (الكرسي) ni mahali pa kuwekea miguu miwili, na ´Arshi hakuna yeyote awezaye kuikadiria isipokuwa Allaah.”[1]

Wapokezi wake ni waaminifu.

[1] Swahiyh. Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “Kitaab-ut-Tawhiyd”, ad-Daarimiy katika “ar-Radd ´alaal-Mariysiy”, Abu Ja´far bin Abiy Shaybah katika “Kitaab-ul-´Arsh” na ´Abdullaah bin Ahmad katika “Kitaab-us-Sunnah” kupitia kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Ammaar ad-Duhniy, kutoka kwa Muslim al-Batwiyn, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh na wapokezi wake wote ni waaminifu. Yuusuf bin Abiy Ishaaq aliifuata kutoka kwa ´Ammaar ad-Duhniy. Ameipokea Abush-Shaykh katika “al-´Adhwamah”. Inatiwa nguvu kwake kupitia upokezi unaotoka kwa Abu Dharr, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 102
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy