47. Du´aa kwa ambaye anatua mahali fulani

130 – Khawlah bint Hakiym as-Sulamiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Akatakapotua mmoja wenu mahali fulani basi aseme:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ الله التامَّاتِ من شَرِّ مَا خَلَقَ

“Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia dhidi ya maovu Aliyoyaumba.”

hakitomdhuru kitu mpaka atapoondoka mahali hapo.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii ndani yake kuna fadhilah za du´aa hii wakati wa kutua mahali. Msingi ni kwamba anayasema haya anapokuwa safarini. Ni lazima kwake kuzingatia na kutafakari Dhikr hii na amdhanie Allaah (´Azza wa Jall) vyema. Hakika hakitomdhuru kitu mpaka atakapotoka mahali pake hapo. Ni sawa pia akiyasema hayo katika sehemu za nyumbani anazokaa mara kwa mara, jangwani au ndani ya gari. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakitomdhuru kitu mpaka atapoondoka mahali hapo.”

Hata kama atachomwa na nge.

[1] Muslim (2708).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 127
  • Imechapishwa: 10/11/2025