47. Allaah alikuwepo na hakukuwepo kitu kabla Yake

44 – Kisha akapokea kutoka kwa Sa´d, ambaye amesimulia kuwa ´Imraan amesema:

”Nilikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati kundi la watu kutoka katika Banuu Tamiym lilipomjia. Akasema: ”Zipokeeni khabari njema, ee Banuu Tamiym!” Wakasema: ”Umetubashiria, hivyo tupe basi!” Likaingia kundi la wayemeni. Akasema: ”Zipokeeni khabari njema, enyi watu wa Yemen, kwani Banuu Tamiym hawakuzikubali.” Wakasema: ”Tumezipokea. Tumekujia ili tupate kuielewa dini na kukuuliza juu ya mwanzo wa jambo hili.” Akasema: ”Allaah alikuwepo na hakukuwa chochote kabla Yake. ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji. Akaziumba mbingu na ardhi na akaandika kwenye Ukumbusho kila kitu.” Halafu akanijia bwana mmoja na kusema: ”Ee ´Imraan! Kamshike ngamia wako ameenda.” Nikaondoka kumtafuta na nikamuona yuko mbali. Naapa kwa Allaah natamani endapo angekimbia na nisingesimama.”[1]

Napata uzito pindi ninapotaja dalili zote hizi kwa lengo la kusimamisha hoja. Hujamsikia mshairi akisema:

Hakuna kitu kinachokuwa sawa katika akili

ikiwa mwanga wa mchana unahitaji kufahamishwa?

[1] al-Bukhaariy (7418).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 102
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy