1- Maana ya unafiki kilugha imechukuliwa kutoka katika “an-Naafiqah”. Ni moja katika matokeo ya aina ya panya kutoka katika shimo lake. Anapotafutwa kupitia njia moja basi hukimbia na kutokezea kwengine. Imesemekana vilevile kwamba imetokana na neno “an-Nafaq” ambayo ni kama pango ambapo mtu hujificha ndani yake[1].
Ama unafiki Kishari´ah maana yake ni kudhihirisha Uislamu na kheri na kuficha ukafiri na shari. Ameitwa hivo kwa sababu anaingia katika Shari´ah kupitia mlango mmoja na anatoka ndani yake kupitia mlango mwingine. Kujengea juu ya hayo Allaah (Ta´ala) amezindua hilo kwa kusema:
الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ
“Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake wenyewe kwa wenyewe, wanaamrisha maovu na wanakataza mema na hufumba mikono yao; wamemsahau Allaah, basi Naye amewasahau. Hakika wanafiki wao ndio mafasiki.”[2]
Bi maana ni wenye kutoka katika Shari´ah.
Allaah akawafanya wanafiki ni waovu zaidi kuliko makafiri. Amesema:
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ
“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni.”[3]
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ
“Hakika wanafiki wanafikiri wanamhadaa Allaah na hali Yeye ndiye Mwenye kuwahadaa.”[4]
يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ
“Wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawazihadai isipokuwa nafsi zao na wala hawahisi. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah akawazidishia maradhi na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.”[5]
[1] an-Nihaayah (05/98) ya Ibn-ul-Athiyr.
[2] 09:67
[3] 04:145
[4] 04:142
[5] 02:09-10
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 90
- Imechapishwa: 16/03/2020

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 90
Imechapishwa: 16/03/2020
https://firqatunnajia.com/46-sura-ya-nne-maana-ya-unafiki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)