199 – Kaamil bin Twalhah ametukhabarisha: Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimwambia ´Umar: “Je, huridhii wao kuwa na dunia na sisi Aakhirah?”[1]

200 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: Sufyaan bin ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd na ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Hind, kutoka kwa Umm Salamah, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pengine ambaye amevaa duniani akawa uchi siku ya Qiyaamah.”[2]

201 – ´Amr bin Shu´ayb ametukhabarisha: Bishr bin Shu´ayb ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Hind, kutoka kwa Umm Salamah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pengine ambaye amevaa duniani akawa uchi siku ya Qiyaamah.”

[1] Ahmad (12009). Swahiyh kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (4/175).

[2] al-Bukhaariy (5844).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 14/07/2025