198 – Duhaym ametukhabarisha: Ibn Abiy Fudayk ametukhabarisha: ´Abdul-Malik bin Zayd bin Sa´iyd bin Zayd, kutoka kwa Musw´ab bin Musw´ab bin ´Abdir-Rahmaan, ambaye amesema:

“Nilimwambia Ibn Shihaab: “Ee ami! Hakika ninasumbuliwa na sciatica. Je, unaweza kunipatia sehemu katika ardhi yako.” Akasema: “Utaifanya nini? Nashuhudia ya kwamba nilimsikia Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan akihadithia kutoka kwa baba yake, ambaye alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akisema: “Pambo la dunia litaondolewa katika mwaka wa 125.”[1] Ibn Shihaab amesema: “Unatarajia nini kutoka kwa kitu ambacho pambo lake limeondolewa?”

[1] Abu Ya´laa (851) na Ibn Abiy Shaybah (7/529). al-Haythamiy amesema:

“Ameipokea Abu Ya´laa na al-Bazzaar. Humo yumo Musw´ab bin Musw´ab, ambaye alikuwa dhaifu.” (Majma´-uz-Zawaa’id (7/257))

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 51
  • Imechapishwa: 14/07/2025