43. Hakuna tofauti kati ya kuabudu masanamu na Mitume waliokufa

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Akikwambia: “Aayah hizi ziliteremshwa kwa wale waliokuwa wanaabudia masanamu! Vipi mtawafanya watu wema ni kama masanamu? Au vipi mtawafanya Mitume ni kama masanamu?” Mjibu kwa yaliyotangulia.

MAELEZO

Washirikina wanamaanisha kuwa Aayah hizi zimeteremshwa juu ya wale wenye kuabudia masanamu na kwamba mawalii hawa sio masanamu. Mjibu kwa njia iliyotangulia: kila mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah, amefanya kile anachokiabudu kuwa ni sanamu. Kuna tofauti baina ya mwenye kuabudu sanamu na mwenye kuwaabudu Mitume na mawalii? Hakuna hata mmoja katika wao anayeza kuwanufaisha wale wanaomwabudu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 61
  • Imechapishwa: 12/11/2023