42. Zakaah ya wanyama waliochanganyika

Ikiwa ndani ya mifugo kuna wazima na wagonjwa, madume na majike, wadogo na wakubwa, basi atatoa mnyama mkubwa aliye mzima ambaye thamani yake inalingana na thamani ya aina mbili za mali hizo.

Ikiwa ndani yake kuna ngamia wa Bukhti na ngamia wa Kiarabu, ng´ombe na nyati, mbuzi na kondoo, walio bora na walio duni, walionenepa na waliokonda, basi huchukua kutoka katika aina mojawapo kwa kiwango kinacholingana na thamani ya mali hizo mbili.

Ikiwa kundi la watu litachanganya mifugo yao katika kiwango cha kinachowajibisha kutoa zakaah cha mifugo inayolishwa malishoni kwa muda wa mwaka mzima, na ikawa malisho yao, dume wao wa kupandisha, mahali pao pa kulala, mahali pao pa kukamulia na sehemu yao ya kunyweshea vikiwa ni kitu kimoja, basi hukumu ya zakaah yao ni kama hukumu ya zakaah ya mtu mmoja. Ikiwa kiwango cha zakaah kitachukuliwa kutoka katika mali ya mmoja wao, basi atarudi kwa washirika wake katika mchanganyiko huo kwa sehemu zao za zakaah hiyo. Kuchanganya mifugo hakuathiri isipokuwa katika mifugo inayolishwa malishoni.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 36
  • Imechapishwa: 26/10/2026