Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Kisha mtu anasema:
أعوذُ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
“Najilinda kwa Allaah kutokamana na Shaytwaan aliyefukuzwa na kuwekwa mbali.”
Maana ya:
أعوذُ بِٱللَّهِ
“Najilinda kwa Allaah… “
bi maana ninaomba kinga na msaada Kwako, ee Allaah.
Maana ya:
مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
“… kutokamana na Shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”
bi maana aliyefukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Allaah, kutokana na kunidhuru duniani na Aakhirah.
MAELEZO
Baada ya du´aa ya kufungua swalah na kabla ya kuanza kusoma aombe kinga kwa Allaah, jambo ambalo limetajwa na Shaykh na kulipambanua. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[1]
Kwa maana unapotaka kuisoma. Ibn Kathiyr amesema katika tafsiri ya Aayah hii:
“Hii ni amri ya kupendeleza si ya lazima. Abu Ja´far Ibn Jariyr na maimamu wengine wamepokea kauli ya maafikiano kuhusu hilo.”
[1] 16:98
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 46
- Imechapishwa: 02/06/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Kisha mtu anasema:
أعوذُ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
“Najilinda kwa Allaah kutokamana na Shaytwaan aliyefukuzwa na kuwekwa mbali.”
Maana ya:
أعوذُ بِٱللَّهِ
“Najilinda kwa Allaah… “
bi maana ninaomba kinga na msaada Kwako, ee Allaah.
Maana ya:
مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
“… kutokamana na Shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”
bi maana aliyefukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Allaah, kutokana na kunidhuru duniani na Aakhirah.
MAELEZO
Baada ya du´aa ya kufungua swalah na kabla ya kuanza kusoma aombe kinga kwa Allaah, jambo ambalo limetajwa na Shaykh na kulipambanua. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[1]
Kwa maana unapotaka kuisoma. Ibn Kathiyr amesema katika tafsiri ya Aayah hii:
“Hii ni amri ya kupendeleza si ya lazima. Abu Ja´far Ibn Jariyr na maimamu wengine wamepokea kauli ya maafikiano kuhusu hilo.”
[1] 16:98
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 46
Imechapishwa: 02/06/2026
https://firqatunnajia.com/40-mapendekezo-ya-kuomba-kinga-kabla-ya-kuanza-al-faatihah/